Home Habari za michezo WAKATI MWANAYE AKIWA KAFUNGIWA NA TFF…MZEE MANARA AVUNJA UKIMYA YANGA… AMTAJA ...

WAKATI MWANAYE AKIWA KAFUNGIWA NA TFF…MZEE MANARA AVUNJA UKIMYA YANGA… AMTAJA MAYELE …


Gwiji wa soka la Tanzania, Yanga SC na Taifa Stars Sunday Manara ‘Computer’ alisema wazi kuwa straika wa Yanga, Fiston Mayele ni mchezaji hatari mwenye kila kitu ambacho mshambuliaji anatakiwa kuwa navyo.

Sunday, ambaye ni Baba mzazi wa msemaji wa Yanga aliyefungiwa na TFF Haji Manara, alisema Fiston atawasumbua sana kwenye mpira wa Tanzania, na hata Afrika kwa sababu ana spidi, jicho la goli na uwezo wa kucheza kwenye mazingira ya aina yoyote.

Mzee Sunday alisema: “Mayele siyo mchezaji wa kawaida, ni mshambualiaji mwenye ‘quality’ mtu ambaye anaweza kukimbia na mpira, mchezaji mwenye jicho analitazama goli kabla hajafunga.

“Naona akiwasumbua sana msimu huu hapa nyumbani na hata kwa Afrika, namuona akiendelea kufunga sana kwenye mashindano yote ambayo watashiriki msimu huu.”

Mayele alifunga mabao matatu kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao Yanga wamecheza na Zalan FC wikiendi iliyopita na watu wengi wanatarajia kuona Mayele akiendeleza moto wa kufunga.

SOMA NA HII  MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO MWAKINYO....KAPOROMOKA KWA NAFASI 16 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI...