Home Habari za michezo TAIFA STARS KUKUTANA NA BALAA LA MASTAA A MOROCCO

TAIFA STARS KUKUTANA NA BALAA LA MASTAA A MOROCCO

Morocco imeita wachezaji 14 kati ya 26 walioshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka jana kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 21.

Kocha wa Morocco, Walid Regragui amechagua mastaa wengi walioiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka jana huko Qatar wakiongozwa na nyota wa PSG, Achraf Hakimi.

Kundi kubwa la nyota hao waliocheza Kombe la Dunia ni wale wa nafasi ya ulinzi na kiungo huku katika ushambuliaji wakiitwa Hakim Ziyech na Ezzalzouli Abde ambao walikuwepo katika kikosi cha dhahabu kilichoandika historia ya kutinga nusu fainali kwa Morocco ambalo lilikuwa taifa la kwanza la Afrika kufanya hivyo.

Nyota watatu tu wanaocheza sokala kulipwa Afrika ndio walioitwa kikosini ambao wote wanacheza kwao Morocco nao ni kipa wa FUS Rabat, Benabid El Mehdi, kiungo Yahya Jabrane na beki Ayoub El Amloud.

Kikosi hicho cha wachezaji 25 wa Morocco ambacho kitacheza na Taifa Stars katika mechi hiyo ya kundi E kinaundwa na makipa Yassine Bounou, Munir el Kajoui na El Mehdi.

Mabeki ni Achraf Hakimi, El Amloud Ayoub, Nayef Aguerd, Ghanem Saiss, Noussair Mazraoui, Yunis Abdelhamid, Yahya Attiat Allah na Abqar Abdelkabir.

Viungo walioitwa ni Richardson Amir, Sofyan Amrabat, Bilal el Khannouss, Ismail Saibari na Jebrane.

Upande wa washambuliaji kuna Ziyechi Hakim, Adli Amine, Ayoub el Kaabi, En-Nesyri Youssef, Tissoudali Tarik, Sofiane Diop, Harit Amine na Ezzalzouli Abde.

SOMA NA HII  MGUNDA,ROBERTINHO WAIRARUA DYNAMO