Home Habari za michezo HERSI ATUA KAIZER CHIEFS KWAAJILI YA MIAMB HII

HERSI ATUA KAIZER CHIEFS KWAAJILI YA MIAMB HII

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said yupo nchini Afrika Kusini ametembelea klabu ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo (PSL)

Katika ukurasa wake wa Instagram Hersi ameposti picha mbali mbali akiwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo akiwemo mmiliki wa klabu ya Kaizer na muanzilishi wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini Premeir Soccer League 1996, Kaizer Motaung.

Motaung aliwahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za soka nchini humo akiwa kama mjumbe wa kamati utendaji ya SAFA (South African Football Association) na pia mjumbe wa kamati iliyoipa nafasi Afrika Kusini Kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2010.

“Faraja yangu kukutana na nguli wa mpira hapa Bondeni na barani Afrika Kaizer Motaung’

Pia, Rais yupo mbioni kukamilisha usajili wa Elie Mpanzu (kiungo mshambuliaji)
Ranga Chivaviro (mshambuliaji wa kati) baada ya kuomba kuondoka Kaizer.

Hata hivyo Hersi anatarajiwa kuhudhuria mchezo wa Ligi kuu huko Afrika Kusini ikiwa ni mchezo wa Soweto Dabi kati ya wenyeji Kaizer Chiefs dhidi ya Orlando Pirates utakaochezwa Uwanja wa FNB saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

“Leo nitakuwa kwenye Dabi ya Soweto kuwaunga mkono Kaizer Chiefs.”

SOMA NA HII  SITA WAPIGWA CHINI JUMLA NDANI YA KMC