Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….MGUNDA ADUKUA MAJINA YA WAANGOLA WATATU…NI VIFAA TUPU…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….MGUNDA ADUKUA MAJINA YA WAANGOLA WATATU…NI VIFAA TUPU…

Kikosi cha Simba kimeendelea kujifua kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Primeiro de Agosto ya Angola, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda akifanya ujanja flani kwa kuondoka na majina matatu ya wapinzani wao mara baada ya mechi ya ugenini wikiendi iliyopita.

Simba ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini mjini Luanda, Angola lakini kabla ya kurejea nyumbani benchi la ufundi chini ya Mgunda, liliondoka na majina matatu ya nyota wa Agosto, ili kuyafanyia kazi kabla ya kurudiana nao wikiendi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mgunda aliondoka na majina ya John Mano, Dago Tshibamba kiungo mshambuliaji aliyefunga bao la kufutia machozi kwa penalti na Vidinho ambao walikuwa mwiba kwenye mchezo huo wa ugenini huku akipania kishindo cha aina yake kuipeleka Simba hatua ya makundi.

Akizungumza Mgunda alisema mechi haijaisha licha ya ushindi mnono wa ugenini na kukiri wachezaji hao watatu waliwasumbua kwenye mchezo wa ugenini na wamejipanga mapema kuwadhibiti baada ya kuondoka na majina yao na kuwasoma kwa ukaribu tangu warejee nyumbani.

Mgunda alisema ameanza kuzifanyia kazi kila dosari zilizojitokeza kwenye mchezo wa kwanza ikiwamo usumbufu wa nyota hao wa Agosto, kupitia mazoezi yanayoendelea kabla ya mchezo huo wa Jumapili, huku mashabiki wa Msimbazi wakiwa na mzuka mwingi wa kutaka kuiona timu hiyo ikiendeleza moto.

“Wachezaji hao ni wazuri na walionyesha ushindani mkali dhidi yetu tunafanyia kazi ili tuweze kupata matokeo mazuri na kuendelea kusonga hatua inayofuata haitakuwa rahisi kwani tunaamini na wao wametambua ubora na udhaifu wetu wanafanyia kazi,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Ubora wa mastaa hao watatu ni namna wanavyocheza kwa akili, kasi na wanacheza kwa nafasi waliweza kumudu mchezo vizuri mbinu na ubora wetu ndio kitu kilichotubeba na kutupa matokeo tuliyoyapata hayajatufanya tubweteke tunaendelea kujianda vizuri ili kuendeleza ubora na kutinga hatua inayofuata.”

Mgunda alisema hawawezi kuandaa mbinu ya kuwadhibiti wachezaji watatu pekee waliowapa changamoto na badala yake wanajiandaa kuikabili timu nzima lakini wakiwazingatia zaidi nyota hao ambao walionekana kuwa tishio.

Mgunda alisema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri waliwasoma wapinzani wao ambapo walipata matokeo mazuri hivyo wanajipanga ili waweze kuonyesha uwezo wao.

Alisema Agosto ni timu nzuri ina wachezaji wengi wazuri, ila hata Simba ni bora ndio maana ilipata matokeo mazuri ugenini na mechi ya marudiano itaingia uwanjani ikiwaheshimu wapinzani ili kuona wanavuka salama kwenda makundi.

SOMA NA HII  KISA KUIFUNGA YANGA GOLI TATU MWENYEWE...AZAM FC WAZIDI KUPAGAWA NA SOPU....MSEMAJI WAO KAIBUKA NA HILI JIPYA...