Home Azam FC UNAKUMBUKA USHINDI WA 4-3 WALIOPATA AZAM FC JANA…BASI HAYA NDIYO YALIYOTOKEA …

UNAKUMBUKA USHINDI WA 4-3 WALIOPATA AZAM FC JANA…BASI HAYA NDIYO YALIYOTOKEA …

USHINDI wa mabao 4-3 walioupata Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini, Uwanja wa Manungu, Morogoro una maana ya kuwapandisha kileleni kuongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 23.

Ukiachana na kuongoza Ligi Kuu ikiwa imecheza mechi 11 imeshinda saba, sare mbili, imefungwa michezo miwili, ina mabao ya kufunga 16 ya kufungwa matano, pia imeifanya Mtibwa Sugar mnyonge wake.

Mtibwa Sugar inakuwa mteja kwa Azam FC baada ya msimu uliopita kupigwa ndani nje, mechi ya Mei 21, 2021/22 ilishinda mabao 2-1(Manungu), Novemba 30 ilipigwa 1-0 (Chamazi).

Pia straika Azam FC, Idris Mbombo ndiye aliyefunga mara ya mwisho na amewafunga leo, mabao mawili dakika ya 17,29, mabao mengine yamefungwa na Abdallah Salum dakika 40 na Daniel Amour dakika 63.

Lakini kwa upande wa Mtibwa Sugar, matokeo hayo siyo mazuri kwao, imecheza mechi 11, imeshinda nne, sare tatu, imefungwa minne, mabao ya kufunga 13 ya kufungwa 20 imevuna pointi 15.

Katika mchezo huo, uliomalizika kwa mabao 4-3 wafungaji ni Adam Adam dakika ya 61, 71 na Nassor Kiziwa dakika ya 76.

Matokeo ambayo kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amezungumzia kwamba licha ya kurejea kipindi cha pili kwa kasi, lakini bahati haikuwa upande wao na anajisikia vibaya kupoteza nyumbani.

Azam inaongoza kwa pointi 23, Yanga 20 na Simba ina 18 na inacheza leo saa 1:00 usiku dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, endapo ikishinda itakuwa na pointi 21 na itashika nafasi ya pili.

SOMA NA HII  POWER DYNAMO HOFU YATANDA ISHU IKO HIVI