Home Habari za michezo WAKATI MORRISON AKITOLEWA YANGA…MAKAMBO NNJE MWEZI MZIMA…DJUMA NA FARID NAO YAWAKUTA…

WAKATI MORRISON AKITOLEWA YANGA…MAKAMBO NNJE MWEZI MZIMA…DJUMA NA FARID NAO YAWAKUTA…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga imesema imejiandaa vyema kuwakabili wapinzani wao Dodoma Jiji katika mchezo wa kesho, Jumanne, Novemba 22, 20222 utakaopigwa katika Dimba la Liti mjini Singida.

Hayo yamesemwa leo na Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Nasredine Nabi wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo huku akiwataja wachezaji watakaoukosa mchezo huo kesho kwa sababu mbalimbali.

“Ukizingatia tumetika kucheza na Singida Big Stars kule Dar, tukasafiri mpaka Dodoma kisha tukaja hapa Singida. Jambo kubwa lilikuwa ni ku-recover miili ya wachezaji na kufanya mazoezi mepesi.

“Mimi na Nabi tulipata nafasi ya kuwatazama Dodoma wakicheza na KMC pale Dar ili kupata analysis ya mtu tunayeenda kuceza naye, tunaamini tupo vizuri na wachezaji wapo vizuri kiafya.

“Mchezaji aliyeumia ni makambo, amepata fructure kwenye mguu na atakaa nje ya uwanja kwa muda usiopungua mwezi mmoja. Wengine ni Aziz Ki ambaye anamalizia adhabu yake kesho, Morrison naye amepata tatizo kidogo lakini sio kubwa, Djuma Shaban na Farid Musa,” amesema Nabi.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI 'THANK YOU' YA ONYANGO...AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO...