Home Habari za michezo A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOWEKA REKODI HII MPYA JANA …CHAMA KAPITILIZA AISEE…

A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOWEKA REKODI HII MPYA JANA …CHAMA KAPITILIZA AISEE…

Simba SC

Simba SC imeendeleza ubabe mbele ya KMC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ushindi huo ni wa tisa kwa Simba SC mbele ya KMC katika michezo 10 waliyokutana tangu mwaka 2018 huku KMC ikiambulia sare moja.

Ushindi  wa jana unaihakikishia Simba pointi saba katika michezo yake mitatu ya Kanda ya Ziwa baada ya kuichapa Geita Gold 5-0 na sare ya 1-1 na Kagera Sugar ikifunga mabao tisa na kuruhusu mawili.

Baada ya ushindi huo, Simba inafikisha mchezo wa tano ugenini bila kupoteza, ikiichapa Polisi Tanzania 3-1, Coastal Union 3-0, Geita Gold 5-0, Kagera Sugar 1-1 na 3-1 mbele ya KMC.

Nahodha, John Bocco ameifungia Simba bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia krosi ya Shomari Kapombe. Bao hilo ni la sita kwa Bocco msimu huu katika ligi.

Simba SC ilipata bao la pili dakika ya 54 kupitia kwa Agustine Okrah kwa shuti kali baada ya kipa wa KMC, David Kissu kutema mpira akiokoa hatari langoni mwake.

Dakika ya 73, Beki Henock Inonga raia wa Congo DR ambaye juzi ameongezewa mkataba na klabu yake hadi mwaka 2025, akaifungia Simba SC bao la tatu kwa kichwa akiunganisha mpira wa kutengwa nje ya eneo la 18 ambao umepigwa na Clatous Chama. KMC ikasawazisha kupitia Sadala Lipangile dakika ya 51 akimalizia krosi ya Kenny Ally.

Bao hilo ni la pili kwa Inonga akifunga katika mechi mbili mfululizo baada ya kuisawazishia kwa kichwa Simba katika sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar, huku assisti aliyotoa Chama ikiwa ya 10 msimu huu kwenye ligi akiwa kinara wa pasi za mabao.

Simba SC imefikisha pointi 41 na kuvuna ushindi wa 12 msimu huu, ikipata sare tano na kupoteza moja, ikifunga mabao 40 na kuruhusu tisa. KMC imebaki kwenye nafasi ya nane na pointi 22 ikishinda mechi tano, sare saba na kupoteza tano, ikifunga mabao 16 na kuruhusu 18.

SOMA NA HII  BINGWA NBC PREMIER LEAGUE KULAMBA MILIONI 600...KOMBE JIPYA LATAMBULISHWA...YANGA WATAKAA NALO SIKU 30 TU...