Home Habari za michezo ACHANA NA STORY ZA VIJIWENI…ILE ISHU YA JOB KUTAKIWA MISRI..UKWELI WOTE HUU...

ACHANA NA STORY ZA VIJIWENI…ILE ISHU YA JOB KUTAKIWA MISRI..UKWELI WOTE HUU HAPA…

Habari za Yanga SC

MASHABIKI wa Yanga walishaanza kupandwa na presha kutokana na taarifa za kitasa wa timu hiyo, Dickson Job kutakiwa na klabu za Al Ittihad Alexandria inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Zoran Maki, lakini beki huyo amewatoa hofu akiwaambia watulie kwa vile bado yupo sana Jangwani.

Job alisajiliwa na Yanga dirisha dogo la msimu wa 2020/2021 akitokea Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili na nusu unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na tangu ametua jangwani amekuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi.

Kiwango alichokionyesha nyota huyo kwenye mechi za ndani na zile za michuano ya CAF ndicho kimemvutia Maki na kutaka huduma ya Job ndani ya Al Ittihad, lakini Mwanaspoti limethibitishiwa kuwa beki huyo ameamua kuwakaushia Waarabu ili asalie Yanga.

Uongozi wa Job chini ya meneja wake, George Job umethibitisha kuwepo kwa ofa zaidi ya moja ikiwemo ya Ittihad na zote zikimhitaji beki huyo, lakini kwa vile bado ana mkataba na Yanga hadi mwisho wa msimu huu wameamua kuanza mazungumazo ya kumpatia mkataba mpya mnono zaidi.

“Kwa sasa mchezaji anapambania timu iweze kutetea taji, juhudi zote kawekeza huko suala la mkataba linazungumzika hii ni kutokana na uwezo wake anaouonyesha. Kuna ofa zaidi ya mbili tunazo, lakini kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga,” alisema George.

“Mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya yameanza, ila sio kwa presha kwani mchezaji anaonyesha kile klabu inataka. Pia nakiri kuwa kwa kiwango alichonacho hakuna timu ambayo haitamani kuwa na beki kama yeye, lakini kubwa mchezaji anazingatia michezo iliyo mbele kuhakikisha anafanya vizuri.”

Yanga chini ya Kocha Nassredine Nabi inaamini katika ubora wa Job na ipo kwenye mipango ya kumpa mkataba mpya ambao huenda ukawa mwaka mmoja kama ambavyo uongozi wake unataka na baada ya hapo ataruhusiwa kutafuta changamoto mpya nje ya nchi.

Sambamba na kuwa katika harakati za kumpa mkataba mpya Job, Yanga pia imepanga kufanya maboresho machache kwenye kikosi chake kwa kuongeza wachezaji wachache na mapendekezo ya kocha Nabi ni kupata beki wa kati kitasa atakayecheza na Job sambamba na kiungo wa kati na mshambuliaji mmoja.

Rais wa Yanga, Hersi Said aligongea nyundo msumari wa Nabi akisisitiza kufanya maboresho ili kuwa na ushindani kwenye michuano wanayoshiriki. “Tuna mpango wa kufanya maboresho machache kwenye kikosi dirisha dogo hili ili timu iwe na ushindani zaidi kwenye ligi na Kombe la Shirikisho Afrika,” alisema Hersi.

SOMA NA HII  YANGA YASHUSHA BEKI HUYU KISIKI KUTOKA SC VILLA