Home Habari za michezo KUHUSU USAJILI MPYA DIRISHA DOGO…SIMBA WATOA TAMKO RASMI…MFUMO UTAKAOTUMIKA NI HUU HAPA…

KUHUSU USAJILI MPYA DIRISHA DOGO…SIMBA WATOA TAMKO RASMI…MFUMO UTAKAOTUMIKA NI HUU HAPA…

Uongozi wa Simba SC umethibitisha kufanya maboresho katika Kikosi chao kupitia Dirisha Dogo la Usajili, kwa kuzingatia mapendekezo ya Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.

Dirisha Dogo la Usajili litafunguliwa rasmi Desemba 15, ambapo Klabu zote za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, zitaruhusiwa kusajili wachezaji ambao wataboresha vikosi vyao.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema, kwa sasa wanasubiri ripoti maalum kutoka katika Benchi la Ufundi ili kufahamu wapi watakapoongeza nguvu kupitia usajili wa Dirisha hilo.

Aidha, amesema wanashukuru wamemaliza salama mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na walichokipata sio haba, hivyo wanaamini Kocha Mgunda na Jopo lake watakuwa na sababu za kutosha kupitia ripoti yao, ili kuushawishi Uongozi kufanya jambo katika usajili.

“Tumemaliza Mzunguko wa Kwanza wa Ligi Kuu, tunamshukuru Mungu kwa tulichokipata, Dirisha Dogo linafunguliwa hivi karibuni na tutafanya maboresho kulingana na Benchi la Ufundi,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTEMANA NA SIMBA...HITIMANA AANIKA SIRI ZA MKUDE..AFICHUA ALIVYOMFUNDA...