Home Habari za michezo TETESI: BAADA YA KULAMBA SHAVU POLISI TZ….ZAHERA AMKUMBUKA MAKAMBO……

TETESI: BAADA YA KULAMBA SHAVU POLISI TZ….ZAHERA AMKUMBUKA MAKAMBO……

Staa wa Yanga SC Makambo atakiwa na Coastal Union

Kikosi cha Polisi Tanzania kimekuwa na msimu mbaya hadi sasa kikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu, kikikusanya pointi tisa tu katika mechi 15, lakini mabosi wa klabu hiyo hawajalala kwani wamempa timu Mwinyi Zahera na kocha huyo fasta amemchomoa straika mmoja kutoka Yanga.

Zahera aliyewahi kuinoa Yanga, ametua Polisi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Joslin Bipfubusa aliyetemwa hivi karibuni na katika moja ya kazi aliyopewa ni kuleta majembe ya kuinusuru timu hiyo kwenye duru la pili na tayari ameshapendekeza jina moja ambalo ni la Heritier Makambo wa Yanga.

Makambo kwa sasa yupo kwao DR Congo alipoenda kwa matatizo ya kifamilia, lakini tayari yupo kwenye rada za Zahera aliyemsajili wakati akiwa Yanga kabla ya kuuzwa AC Horoya ya Guinea na kurejea msimu huu Jangwani, timu ikinolewa na Nasreddine Nabi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Polisi, kimesema, kuwa wamefanya makubaliano na mabosi wa Yanga ili wawaachie mshambuliaji huyo, aliyemaliza na mabao 17 msimu wa 2018-2019 nyuma ya Meddie Kagere aliyekuwa na Simba na Salim Aiyee aliyekuwa Mwadui.

Makambo alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili msimu uliopita akitokea Horoya lakini hajawa na makali kiasi cha kukosa namba mbele ya Fiston Mayele katika kikosi cha kwanza na Zahera aliyekuwa mkurugenzi wa soka la Vijana Yanga amewakodeza Polisi kuwa yeye anamjulia straika huyo.

Inaelezwa Zahera amewahakikisha Polisi wakimchukua Makambo akaungana na kina Vitalis Mayanga na wenzao waliopo kikosini atafanya makubwa kwani anajua namna ya kumtumia kama alivyofanya alipokuwa naye Yanga na kufunga mabao ya kutosha katika msimu wa kwanza tu Jangwani.

“Mazungumzo na uongozi wa Yanga yanakwenda vizuri tunatarajia mchezaji ataweza kukubaliana na ofa yetu kutokana na Zahera kuongeza nguvu kwenye mchakato huo,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake litajwe, kichoongeza:

“Mbali na usajili huo kama utakamilika bado tutaongeza kiungo mkabaji na mshambuliaji na safu ya ulinzi itaongezewa nguvu lengo ni kuunda kikosi kitakachotoa ushindani katika duru la pili na kuisaidia timu iweze kubaki Ligi Kuu.”

SOMA NA HII  KUPITIA SIMBA TANZANIA KUWEKA REKODI MPYA KWA MKAPA...MASHINE YA VAR KUFUNGWA...CAF WABARIKI...