Home Habari za michezo BAADA YA KUPEWA KAZI KUBWA YANGA…MUDATHIRI AOMBA POO…AFUNGUKA ISHU YAKE NA SURE...

BAADA YA KUPEWA KAZI KUBWA YANGA…MUDATHIRI AOMBA POO…AFUNGUKA ISHU YAKE NA SURE BOY..

Habari za Yanga

Siku chache baada ya kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kukiri kuwa kiungo wake ambaye anajua kukaba na kutengeneza mashambulizi, Mudathir Yahya ameomba kupewa muda zaidi ili kuonyesha ubora wake, naye amefunguka.

Nabi alisema kuwa amepata kiungo bora ambaye anatamani kumtengeneza zaidi ili aweze kuwa na maamuzi ya haraka awapo eneo la kufunga kama ilivyo kwa Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Hata Hivyo, akizungumza na Mwanaspoti, Mudathir alisema anafurahia maisha ndani ya timu hiyo ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza moja kwa moja kitu ambacho hakukitarajia.

“Nimetoka nje ya uwanja kwa muda kutokana na kukosa timu baada ya kumaliza mkataba na waajiri wangu wa zamani Azam FC, nilikuwa nafanya mazoezi lakini sikuwa nacheza mechi za ushindani ambazo zingeweza kunipa utimamu wa mwili hivyo kupata namba kikosi cha kwanza ni njia ya kunirudisha haraka,” alisema na kuongeza;

“Nimekuwa nikipokea pongezi nyingi za kile ninachokifanya lakini naomba kuweka wazi kuwa bado sipo fiti nahitaji muda zaidi ili niweze kuonyesha mambo mengine bora na kuisaidia timu yangu kufikia malengo.”

Akizungumzia kucheza pamoja na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ alisema ni faraja kwake kuungana tena na kiungo huyo ambaye wamefanya kazi pamoja na kupata mafanikio wakiwa Azam FC.

“Kucheza pamoja na Sure Boy imenirahisishia zaidi kuonyesha ubora, kwani ni mchezaji ambaye ananifahamu na mimi pia namfahamu hivyo tunafichiana mapungufu naamini kadiri muda utakavyokuwa unakwenda tutafanya kwa ubora zaidi,”

“Kupotezana kwa muda na kukutana tena ni suala ambalo linaongeza imani ya kujiweka fiti zaidi ili tuiweze kuendeleza ubora ambao tuliuonyesha nje ya Yanga.”

Pia alizungumzia malengo yake kuwa ni kuhakikisha anaipambania timu hiyo kutetea taji walilolishikikia na yeye kunyanyua kwapa kwa muda mwingine baada ya kufanya hivyo 2013/14, akiwa na Azam FC.

SOMA NA HII  ISHU YA UWEKEZAJI MO DEWJI NA SIMBA YAFIKA BUNGENI..."MWEKEZAJI ANALETA JANJA JANJA