Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MUSONDA NA MAJERAHA…YANGA WAIBUKA NA TAARIFA MPYA…KUMBE NI…

KUHUSU ISHU YA MUSONDA NA MAJERAHA…YANGA WAIBUKA NA TAARIFA MPYA…KUMBE NI…

Habari za Yanga

Kwenye mchezo wa juzi kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting, Kennedy Musonda alitoka uwanjani akichechema baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji Shabani Msala wa Ruvu Shooting.

Hofu ya mashabiki wa Yanga ikawa kwenye kutaka kujua hali ya mchezaji huyu baada ya mchezo ule ambapo Msemaji wa Wanannchi, Ally Kamwe amesema mshambuliaji huyo yuko fiti.

“Tumezungumza na madaktari wetu wakiongozwa na Moses Etutu, wametuthibitishia kuwa Kennedy Musonda yuko fiti, hakupata tatizo kubwa, ilikuwa mgongano tu wa kawaida kwenye soka.

“Baada ya pale alikuwa sawa kabisa na leo wachezaji wote tuliowasajili wamepelekwa checkup kwa ajili ya taratobu zingine za msimu. Musonda yuko fiti kwa hiyo mashabiki na wanachama wa Yanga wasiwe na wasiwasi,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  ISHU YA KOCHA WA SIMBA KUONDOKA KAMBINI IKO HIVI.... ROBERTINHO AFUNGUKA KILA KITU