Home Habari za michezo SIMBA WAZIDIWA NGUVU USAJILIWA KIFAA HIKI CHA KAZI…ATUA KWA TIMU NYINGINE KIULAINIII…

SIMBA WAZIDIWA NGUVU USAJILIWA KIFAA HIKI CHA KAZI…ATUA KWA TIMU NYINGINE KIULAINIII…

Habari za Simba

Mabosi wa Simba walishakamilisha kila kitu hadi kwenye masuala ya kimaslahi kuhusu dili la kumsajili kiungo wa ulinzi wa Geita Gold, Kelvin Nashon na kilichokuwa kimebaki ni utekelezaji tu, lakini kiungo huyo ameyeyuka na sasa ametua Singida Big Stars.

Uongozi wa Simba ulitakiwa kutuma mkataba kwa Nashon ili ausome na kama kuna sehemu alikuwa haridhiki nayo urekebishwe vile ambavyo anahitaji ili aweze kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Katika mazungumzo na viongozi wa juu Simba, walikubaliana na Nashon kumsainisha mkataba wa miaka mitatu pamoja na maslahi mengine kama mshahara, pesa ya usajili na kulipa kiasi cha pesa kwa uongozi wa Geita kwani amebakiwa na mkataba wa miezi sita.

Taarifa kutoka ndani ya Geita zinasema ni kwamba Simba imemkosa Nashon kutokana na dau waliloweka Singida Big Stars.

Awali, uongozi wa Singida, Januari 3, ulituma barua iliyoonyesha maombi ya ruhusa ya kuzungumza na Nashon kwani walikuwa kwenye mipango yao ya usajili baada ya kupendekezwa na benchi lao la ufundi lililokuwa chini ya kocha Hans Pluijm na leo imefahamika mambo yamekamilika.

Hii ni baada ya uongozi wa Geita kukubalii maombi hayo ya Singida na Nashoni akasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo na kuungana na kiungo mwingine wa timu hiyo aliyemfuata Pluijm, Yusuph Kagoma.

‘Muvi’ zima la Singida kumsajili Kagoma lilichukua siku tatu hadi nne kukamilika kwa kila kitu na kwenda naye mchezaji kwenye Kombe la Mapinduzi.

Mwenyekiti wa Geita, Leonard Bugomola alisema ni kweli wamepokea barua kutoka Singida ikionyesha nia ya kuhitaji kufanya mazungumzo na Nashon kisha wakikubaliana iweze kumsajili kama ilivyofanya kwa Kagoma ambaye tayari wamempata.

“Katika timu yetu sio Nashon tu ila karibu wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wameombwa na timu mbalimbali ingawa hatuwezi kukubali kuwaachia wote,” alisema Bugomola na kuongeza;

“Wale waliokuwa ndani ya uwezo wetu tutaongea nao na kuwapatia yale maslahi wanayohitaji ili kuweza kuwabakisha kwenye kikosi chetu na naamini hilo linawezekana.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUCHOONGA SANA SAFARI HII..SIMBA WAIHENYESHA KWA MIAKA 10...ISHU IKO HIVI...