Home Habari za michezo YANGA WAMZIDI UJANJA BIGIRIMANA….BADALA YA KUMLIPA MIL 700…WATAMPA NUSU TU….

YANGA WAMZIDI UJANJA BIGIRIMANA….BADALA YA KUMLIPA MIL 700…WATAMPA NUSU TU….

Bigirimana akiwa Yanga SC

Aliyekuwa kiungo wa Yanga raia wa Burundi, Gael Bigirimana amerejea nyumbani kwao Burundi baada ya kuvunjiwa mkataba wake na Klabu ya Yanga.

Yanga ilimchomoa Gael kikosini dakika chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15 na nafasi yake kuchukuliwa na beki kutoka Mali, Mamadou Doumbia lakini staa huyo amewaganda Wanajangwani hao akitaka wamlipe stahiki zake na fidia haraka iwezekanavyo ili aendelee na yake.

Gael kiungo wa zamani wa Newcastle United ya England amekubali kulipwa kwa awamu nne madai ya fedha zake za kuvunja mkataba ambapo mkataba wake na Yanga ulikuwa na kipengele cha kulipa shilingi milioni 700 upande wowote iwapo utaamua kuvunja mkataba.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa, Yanga wametumia kipengele cha kutocheza mechi zaidi ya asilimia 50 tangu ajiunge na klabu hiyo hivyo Yanga wamekubali kulipa nusu (Milioni 350) kuvunja mkataba huo.

Mwanzo Yanga ilitaka Gael aendelee kuwa ndani ya kikosi ili acheze Kombe la Shirikisho Afrika lakini sio ligi baada ya wachezaji 12 wa kigeni kutimia, lakini nyota huyo amegomea jambo hilo.

Gael alisajiliwa Yanga mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, lakini hakuonyesha ubora ambao Wanajangwani hao waliutarajia kutoka kwake jambo lililofanya waachane naye baada ya miezi sita tu na Mwanaspoti limepenyezewa timu hiyo inatahitajika kumlipa kiungo huyo Dola 300,000 (karibu Sh700 milioni).

β€œIlikuwa lazima wamlipe, meneja wake alikuja kutokea England kuonana na uongozi na wamekubali kumlipa kwa mafungu,” chanzo chetu kilieleza.

SOMA NA HII  MZEE MPILI: TUNAIFUNGA SIMBA TENA KIGOMA, MANARA ANIPE MILIONI YANGU