Home Habari za michezo KISA KUKUTANA NA GSM..MWIJAKU AIHAMA SIMBA…ADAI NJAA ILIMSUMBUA…

KISA KUKUTANA NA GSM..MWIJAKU AIHAMA SIMBA…ADAI NJAA ILIMSUMBUA…

Habari za Simba

Mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku ameikana Klabu yake ya Simba na kusema kuwa kuanzia sasa yeye ni shabiki wa Yanga.

Mwijaku amesema hayo leo Jumatatu, Februari 19, 2023 wakati wa Kipindi cha LeoTena cha Clouds FM akimfanyia mahojiano Rais wa Yanga, Eng. Said Hersi.

Kauli hiyo ya Mwijaku inakuja ikiwa ni siku mbili baada ya Simba kuambulia kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Raja Casablanca katika mchezo wa Kundi C wa Klabu Bingwa Afrika huku Yanga wakishinda bao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Hersi: Mwenyezi Mungu ametuhusia kuishi kama ndege , unaamka asubuhi unaenda kutafuta ridhiki unarudi ukiwa na ridhki, Mwijaku ni mtafuta ridhiki.

Mwijaku: Mimi ni Mwananchi, ukizaliwa tu ndani ya nchi hii wewe ni Yanga, Ghalib (GSM ) aliniambia ni njaa inanisumbua

Da Huu: Kwa hiyo wewe ni Yanga?

Mwijaku: Eenh kwani hujamsikia @alikamwe ? Ukizaliwa Tanzania tu wewe ni Yanga.

SOMA NA HII  YANGA WABEBWA TENA SHIRIKISHO....CAF YAPANGUA NJAMA CHAFU ZA WATUNISI...STORI IKO HIVI..