Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA RAJA CASABLANCA..MO DEWJI ASHUSHA FURAHA SIMBA…MASHABIKI KICHEKO TUPU…

KUELEKEA MECHI NA RAJA CASABLANCA..MO DEWJI ASHUSHA FURAHA SIMBA…MASHABIKI KICHEKO TUPU…

Mashabiki Simba

Rais wa Heshima na muwekazaji wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ameagiza kushushwa kwa viingilio vya mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kati ya Simba SC dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi hii ya February 18 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Awali kiingilio cha chini ambapo ni mzunguko kilikuwa Sh. 5000 lakini sasa itakuwa Sh. 3000 wakati VIP C ilikuwa 20,000 na sasa itakuwa Sh. 10,000.

Mo amechukua maamuzi hayo ili kuwafanya mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi Uwanjani kuipa sapoti timu yao ili ifanye vizuri.

Viingilio vipya vilivyopangwa ni kama inavyoonekana hapa chini!

Mzunguko Sh. 3,000 VIP C Sh. 10,000 VIP B Sh. 20,000 VIP A Sh. 30,000.

SOMA NA HII  Infinix NA TIGO WAZINDUA RASMI SIMU KALI YA FUNGA MWAKA.

1 COMMENT