Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA WATUNISIA… MKAKATI WA YANGA ‘KUIPELEKEA MOTO’ MAZEMBE UKO...

BAADA YA KUMALIZANA NA WATUNISIA… MKAKATI WA YANGA ‘KUIPELEKEA MOTO’ MAZEMBE UKO HIVI…

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa habari za Monastir wameziacha Tunisia na sasa malengo yao makuu ni kushinda katika mchezo wao wa Jumapili, Februari 19, 2023 dhidi ya TP Mazembe ya Congo.

Kamwe amesema hayo baada ya kutua Dar es Salaam na kikosi cha timu yake wakitokea Tunisia ambako walicheza na US Monastir na kuambulia kipigo cha bao 2-0 na kusema kuwa malengo yao jkwa sasa ni kusaka alama tatu dhidi ya TP Mazembe.

“Focus yetu ni mchezo wa Jumapili dhidi ya TP mazembe, hii ni group stage kuna michezo sita, tumepoteza mmoja bado mitano, kuna pointi 15 za kugombewa. Ishu ya Monastir tumeimaliza palepale Tunisia, sasa hivi akili yetu imejikita kwa TP Mazembe.

“Mashabiki tuhakikishe tunaujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa, hamasa ziongezeke, safari ndiyo kwanza imeanza na tunaamini tutaondoka na alama tatu Inshallah!

“Sisi tulikuwa angani hakuna mtandao, bahati nzuri wakati tunashuka hapa kuwasha simu zetu tukaona kuna ahadi Mhe. Rais Samia ametoa kwamba kila bao litakalofungwa atatoa Tsh milioni 5.

“Cha kwanza nikamgeukia mshambuliaji wetu, Fiston Mayele nikamwonesha simu kwamba Rais amesema kila goli atatoa Tsh milioni 5, kwa sisi kama timu ya Wananchi lazima tuhakikishe tunashinda na kumpa furaha rais wetu.

“Nimemwambia Mayele, Musonda mpaka Dickson Job na Kibwana kwa sababu mechi ya Jumapili hatuna plan nyingine zaidi ya kushambulia tu. Plan A ni kushambulia, B ni kushambulia na C ni kushambulia. Kwa hiyo linaweza kutokea lolote Kibwana naye akatupia. Tukutane kwa Mkapa.

“Tunawaheshimu TP mazembe ni timu kubwa, kwetu ni mchezo mgumu kwelikweli ndiyo maana tunataka mashabiki wa-play part yao. Sisi hatuna presha na mchezo huu, lakini tupo makini sana kuwakabili Mazembe,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  CHE MALONE:- NATAKA CHANGAMOTO MPYA...HUENDA MSIMU UJAO NIKACHEZA TIMU KUBWA ZAIDI...