Kocha Msaidizi wa Taifa, Hemed Morocco, ametaja sababu ya kumuita Kiungo Mshambuliaji Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kwenye timu ya taifa kuwa ni kutokana na umri wake mdogo.
Morocco amesema kikubwa walichokizingatia ni kujiridhisha kuwa anafanya mazoezi ukiachilia mbali matatizo baina yake na klabu yake ya Yanga SC.
“Ni Mchezaji ambaye anaonekana anafanya mazoezi yuko vizuri na hiki ni kitu cha kupambania Nchi, ukiwa mchezaji mzuri hata kama una matatizo tutakuita, falsafa yetu imeona atatusaidia Feisal ni mdogo na tunapenda Wachezaji wadogo hata kama hawapo katika mechi za ushindani muhimu wanafanya mazoezi tumejiridhisha, ndio maana tumemchagua,” alisema Morocco.
SOMA NA HII BAADA YA KUFUNGWA MAGOLI YA 'KIZEMBE' JUZI....ALLY SALIM AIBUKA NA KUJITETEA KWA HILI...