SIMBA SC KUWAKARIBISHA IHEFU FC...YANGA WAVAANA NA GEITA GOLD...AZAM FC KUWAINGIZA MJINI MTIBWA
news

SIMBA SC KUWAKARIBISHA IHEFU FC…YANGA WAVAANA NA GEITA GOLD…AZAM FC KUWAINGIZA MJINI MTIBWA

Marce Ben Komba March 15, 2023 6:45 pm

Droo ya Michezo ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2022/23, imefanyika mchana huu huku kila Timu ikipata nafasi ya kumjua mpinzani wake.

Robo Fainali ya Kwanza ni Simba SC, ambao watakabiliana na Ihefu huku Simba wakiwa ndio wenyeji wa mchezo huo.

Robo Fainali ya Pili, Singida Big Stars watakuwa nyumbani Uwanja wa Liti kuwakaribisha Mbeya City.

Robo Fainali ya Tatu itakuwa ni Bingwa mtetezi Yanga kwa wakati mwingine wanaikaribisha Geita Gold FC.

Na Robo Fainali ya nne, Matajiri wa Jiji, Azam FC watakuwa nyumbani kuwakaribisha Mtibwa Sugar.

YANGA INAGAWA DOZI NYUMBANI NA UGENINI…GARI LIMEWAKA JANGWANI…MNYAMA HAFUI DAFU ZIZO NA SHALULILE WANYONGE TU…CHAMA “MWAMBA WA LUSAKA” BABA LAO…CAF IMETHIBITISHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply