Baada ya Klabu ya Simba SC kuifunga timu ya Horoya AC kwa bao 7-0 na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champion League),
Tanzania imefanikiwa kuongeza pointi 10 na sasa kufikisha pointi 39 na kuwa na uhakika wa asilimia 100 wa kupeleka timu nne tena msimu ujao.
Aidha, baada ya Klabu ya Yanga SC kufanikiwa kuifunga timu ya US Monastir ya Tunisia jana na kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup),
Tanzania imeongeza pointi 7.5 na kufikisha pointi 46.5 na kupanda kutoka nafasi ya 9 ya Association Ranking mpaka nafasi ya saba na kulifanya Taifa kuwa miongoni mwa taifa lenye nguvu kisoka Afrika.
Point hizo 46.5 zimetengenezwa na vilabu vitatu vya Tanzania kama ifuatavyo;
10 Young Africans
35 Simba
1.5= Namungo
Ndani ya msimu mmoja Yanga imekusanya points (10) yaani. 2.5= Kufuzu makundi 7.5 = Robo fainali
Kutokana na points hizo kwa sasa Tanzania tunashika nafasi ya (7) Afrika.
1. Morocco
2. Egypt
3. Algeria
4. South Africa
5. Tunisia
6. DR Congo
7. Tanzania