Home Habari za michezo HAWA HAPA MASTAA MUHIMU WA YANGA WATAKAOKOSEKANA MECHI NA MAZEMBE…DIARRA NDANI…

HAWA HAPA MASTAA MUHIMU WA YANGA WATAKAOKOSEKANA MECHI NA MAZEMBE…DIARRA NDANI…

Habari za Yanga

Kumekuwa na stori nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Yanga itawakosa wachezaji wake wengi kwenye mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe nchini Congo.

Hii inatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na kupata kadi mbili za njano katika michezo miwili inayofuatana ya michuano hiyo.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya CAF, mchezaji atakosa mchezo unaofuata kwa kupata kadi mbili za njano mfululizo.

Kwa Yanga Djuma Shabani pekee ndiye aliepata kadi mbili za njano katika mechi mbili zilizofuatana, alipata kadi katika mechi ya Real Bamako katika Dimba la Mkapa na mchezo dhidi ya Us Monastir.

Mchezaji mwingine aliyepata kadi ya njano katika mchezo wa Bamako ni mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye mchezo wa pili hakupata kadi.

Lakini katika mchezo wa wikiendi iliyopita kati ya Yanga na Maonastir, wachezaji wa Yanga waliopata kadi ni wanne.

-Djigui Diarra -Djuma Shabani -Ibrahim Bacca -Khalid Aucho

Kwa hiyo kwa kigezo cha adhabu ya kadi ni Djuma Shabani pekee vinginevyo kocha atakua ameamua kuwapumzisha nyota wake.

Au kocha atawapumzisha Djigui Diarra, Khalid Aucho na Ibrahim Bacca dhidi ya Mazembe kwa kuhofia wasije wakapata kadi ya pili itayowafanya wakose mechi ya robo fainali.

SOMA NA HII  HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUHUSU 'KUCHEZA MECHI NNJE YA UWANJA'...MATOKEO YATAJWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here