Home Habari za michezo HIZI HAPA SABABU ZA MSUVA, SAMATTA KUPOTEANA…MBINU KUKWAMA…MECHI YA TANZANIA VS UGANDA

HIZI HAPA SABABU ZA MSUVA, SAMATTA KUPOTEANA…MBINU KUKWAMA…MECHI YA TANZANIA VS UGANDA

HIZI SABABU ZA MSUVA, SAMATTA KUPOTEANA...MBINU KUKWAMA...MECHI YA TANZANIA VS UGANDA

BAO la dakika za majeruhi lililowekwa kimiani na mtokea benchi wa Uganda, Rogers Mato, lilitibua mipango ya Taifa Stars katika safari ya Afcon mwakani nchini Ivory Coast.

Stars ilipoteza mechi hiyo ya marudiano ya Kundi F iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tangu ilipoifunga Uganda kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Ismailia, nchini Misri.

Matokeo hayo ya juzi yameifanya Stars kusaliwa na pointi nne ikiwa nafasi ya pili ikilingana kwa kila kitu na Uganda iliyopo nafasi ya nne kwa tofauti zao za herufu, huku Algeria ikiongoza kundi na kukata tiketi ya kwenda Ivory Coast kwa kukusanya jumla ya pointi 12.

SOKA LA BONGO linakuchambulia dakika 90 za mchezo huo na kuainisha baadhi ya vitu vilivyoitibulia Stars mbele ya Uganda na nafasi iliyosalia kupitia mechi mbili ilizonazo mkononi kabla pazia la makundi kufungwa zitakazochezwa Juni mwaka huu na hatma ya kwenda Afcon kwa mara ya tatu.

MBINU ZAKWAMA

Mabeki wa pembeni Dickson Job na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyeanza sehemu alicheza Dismas Novatus aliyepelekwa kati kucheza na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ walitumika kupelekea mashambulizi hato, wakisaidiana na mawinga Simon Msuva na Abdul Suleiman ‘Sopu’.

Kasi ya Msuva na Sopu iliwapa changamoto kubwa mabeki wa Uganda lakini pamoja na kusumbua bado Stars haikuweza kupata bao, kwani mbinu zote zilikwamba mbele ya mabeki wa The Cranes waliokuwa makini kuondoa kila aina ya hatati.

UGANDA ILITULIA

Ile ya kauli ya kocha wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ kwamba vijana wake wadogo sehemu yao ya kukua ni Uwanja wa Mkapa ilionekana, kwani timu hiyo iliingia na kuwasoma Stars namna ambavyo wanacheza na wao walitulia huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Hakuwa na papara ila ilipofika dakika ya 27 wachezaji wake walianza kufunguka na kwenda langoni kwa Stars.

Washambuliaji wao Richard Basangwa na Emmanuel Okwi walikuwa wanapeleka mashambulizi kwa spidi lakini bado walikumbana na changamoto ya ukuta wa Stars.

UMEME WATIBUA

Wakati pambano likizidi kushika kasi, ghafla likatibuliwa na hitilafu ya umeme iliyofanya taa zififie uwanjani.

Hii ni moja ya tatizo ambalo lilifanya mchezo upoe kwa sababu ilipofika dakika ya 36 waamuzi walisimamisha mechi wakidai mwanga ni hafifu uwanjani.

Mwanzoni wachezaji walionekana wakipasha pasha ili miili isipoe lakini mwisho walitulia baada ya kuona zimepita takribani dakika 38.

Timu zilipoingia uwanjani baada ya mambo kukaa sawa mchezo haukuwa tena na spidi kwa sababu wachezaji walipoa hadi wanaenda vyumbani kwa ajili ya mapumziko.

BATO LA KIUNGO

Stars kwenye eneo la kiungo ilikuwa na Himid Mao, Mudathir Yahya na Mzamiru Yassin ambao walicheza kwa maelewano ya juu.

Mao na Mudathir wao walikuwa wanatumika kwenye kukaba zaidi huku upande wa Mudathir yeye akisambaza mipira.

Upande wa Uganda walikuwa na Khalid Aucho, Isma Mugulusi na Bobosi Byaruhanga.

Aucho na Mugulusi walikuwa wakikaba zaidi huku Bobosi yeye akiwa anasambaza mipira mara kwa mara alikuwa anafanikiwa.

Kwenye ukabaji Aucho na Mugulusi walikuwa na vita kubwa na Mzamiru, Mudathiri na Mao ambao nao walikuwa bega kwa bega kuhakikisha lango lao haliguswi.

Eneo hili lilikuwa kivutio zaidi kwani uchezaji wao kulikuwa na unyumbulifu na ukabaji.

Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha Adel Amrouche ya kuwatoa Himid na Mzamiru na kuwaingiza Feisal Salum na Shomary Kapombe na ile ya Tshabalala ili kumpisha David Luhende ilichangia Stars kupoteza ile kasi yake na kuwahimili nyota wa Uganda na kupoteza mechi.

MSUVA, SAMATTA WAPOTEANA

Washambuliaji wa Stars, Mbwana Samatta na Simon Msuva kwenye kipindi cha pili walipoteana kutokana na mipango yao kutokamilika.

Msuva kuna muda alikuwa anatumia mbinu ya kupiga mpira mrefu na kuukimbilia kwa spidi lakini alijikuta akizuiwa na mabeki wa Uganda.

Huku Samatta naye alikuwa akiipozesha timu wakati zikipigwa pasi za spidi kwa ajili ya kupeleka mashambulizi, kadhalika alikosa umakini katika maamuzi kwenye kupiga mashuti au kutoa pasi na kujikuta Stars ikipoteza nafasi kadhaa ambazo zingeibeba.

Kubanwa kwa Msuva kulitoa fursa kwa Sopu na yeye alikuwa na spidi lakini kuingia ndani ya boksi alikuwa hapati kutokana na kudhibitiwa na mabeki wa Uganda waliokuwa na miili mikubwa kuliko aliyonayo mshambuliaji huyo chipukizi.

Hata Samatta alipotolewa dakika za jioni kumpisha Said Khamis JR, tayari mambo yalikuwa yameshachelewa na ndipo Uganda ikapata bao lililowafanya walipe kisasi cha kupoteza nyumbani.

SUB ZA UGANDA

Tofauti na Adel aliyefanya mabadiliko yaliyoigharimu Stars, kwa upande wa kocha wa Uganda, Micho alibebwa na maamuzi ya kumtoa Okwi aliyepunguza kasi ili kumpisha Rogers Mato kisha Joseph Ochaya kumpisha Travis Mutyaba na baadaye Busangwa kumpisha Fahad Bayo, Faruk Miya kuchukua nafasi ya Ismail Mugulusi kabla ya Bobosi kumpisha Mukwala.

Uganda iliiduwaza Stars kwa bao la dakika ya majeruhi lililofungwa na Mato kwa mpira ulionzia kwa Aucho aliyetoa pasi Miya aliyemtengena mfungaji aliyepiga shuti lililomuacha Aishi Manula akirudi bila mafanikio ya kuuzuia.

NOVATUS, BACCA WAMOTO

Licha ya mikwamo hiyo, lakini katika mechi ya juzi mabeki wa Stars wakiongozwa na Bacca na Novatus walisimama imara na kuonyesha uwezo mkubwa wa kuosha kila aina ya hatari na kuiendesha timu kuanzia nyuma. Beki huyu alionyesha umahiri wa mipira ya juu na hata kucheza rafu zisizo na madhara.

Mchezo uliopita alicheza kama beki wa kushoto na akafanya vizuri. Mchezo huu wa marudiano alisimama beki wa kati na bado alifanya vizuri sambamba na Bacca.

NAFASI BADO IPO

Stars inapaswa kuifunga Niger Dar lakini iombee Uganda ipoteze dhidi ya Niger na Algeria kwani wanalingana nao kwa pointi na hata mabao ya kufunga na kufungwa.

Lakini Uganda ikitetereka Stars ipate pia pointi Jijini Algiers. Hata hivyo ni lazima kazi ifanyike mapema kabla tya mechi hizo za Juni kuweza kuiona Tanzania ikienda fainali za Afcon kwa mara ya tatu baada ya zile za awali za 1980 nchini Nigeria na 2019 zilizofanyika Misri kwa vile nafasi bado ipo na kuteleza siku zote sio kuanguka.

SOMA NA HII  YANGA SC YATOA WAWILI KIKOSI BORA SHIRIKISHO