Home Habari za michezo HUYU HAPA MRITHI WA TSHABALALA SIMBA…AVALISHWA MIKOBA RASMI

HUYU HAPA MRITHI WA TSHABALALA SIMBA…AVALISHWA MIKOBA RASMI

MOHAMED HUSSEIN NA KIBU...WAPIGWA CHINI MECHI NA RAJA CASABLANCA

Wakiwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Raja Casablanca, mikoba ya nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein Zimbwe Jr inatarajiwa kuwa mikononi mwa Gadiel Michael.

Zimbwe atakosekana kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili Mosi, mwaka huu ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi kwa timu hizo mbili ambazo zimetinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa watakosa huduma ya Zimbwe kutokana na adhabu ya kadi za njano, lakini wachezaji wengine wapo tayari.

“Tutakosa huduma ya nahodha msaidizi Mohamed Hussein, lakini wapo wachezaji wengine wapo tayari kutokana na mbinu za mwalimu mwenyewe atakavyoamua kuanza.

“Tukiwa ugenini hatuna hofu kwani licha ya kwamba tumetinga hatua ya robo fainali mchezo wetu dhidi ya Raja Casablanca ni muhimu kupata matokeo mazuri, tutafanya jitihada kubwa kupata matokeo chanya,” alisema.

Gadiel alikuwa chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira tangu Machi 24, mwaka huu kwenye mazoezi yaliyoanza Uwanja wa Simba uliopo Bunju, Dar, yupo kwenye msafara wa kwanza ambao unatarajiwa kuibuka Morocco kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo.

SOMA NA HII  CAF KUAMUA HATMA YA USAJILI SIMBA NA YANGA....MASTAA HAWA HATARINI KUFYEKWA....