Home Uncategorized NAMNA KOCHA WA SIMBA NA GLOBAL GROUP WALIVYOENDELEA KUTOA MISAADA KWA WAHITAJI,...

NAMNA KOCHA WA SIMBA NA GLOBAL GROUP WALIVYOENDELEA KUTOA MISAADA KWA WAHITAJI, LEO ILIKUWA MWANZA



KAMPUNI ya Global Publishers leo imefanikiwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Masjid-Ngamia kilichopo Kangaye,Wilayani Ilemela jijini mwanza.

katika msaada huo Global Publishers ni kwa niaba ya aliyekuwa kocha na mchezaji wa zamani wa Simba Talib Hilali ambaye anaishi Oman ambaye ameamua kusaidia watoto jijini Mwanza.

Kabla Talib Hilal alitoa misaada kama hiyo jijini Dar es Salaam na Global ikafanya kazi ya kufikisha.

Misaada iliyotolewa leo ni Sukari, Unga wa ngano, Mafuta ya kupikia, Maharage pamoja na Ndoo za kutakasa mikono katika kipindi hiki cha kujikinga na virusi vya corona ambavyo vinazalisha ugonjwa wa Covid-19 na i
likabidhiwa na Shabani Ally.

Akizungumza na Spoti Xtra Mama mlezi wa kituo hicho Rehema Shaban amesema kwamba:- ” kwanza napenda kuwapongeza sana Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Talib kwa msaada huu walioutoa.

“Msaada huu utatusaidia kwa mambo mbalimbali kwani kama mlivyoona hatukuwa na ndoo ya kunawia mikono ila tumepata kutoka kwa Talib aliyeshirikiana na Global kutufikishia hii misaada, hivyo tunawapongeza sana. 

“Tunaendesha kituo hiki katika mazingira magumu sana kwani hatupati misaada lakini kwakua ni wito kufanya hii kazi ya kulea hawa watoto yatima tunajikamua wenyewe mifukoni ilimradi siku ziende.

“Misaada hii itatusaidia sana kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo sasa watoto hawa wanaweza kufunga kwakua uhakika wa kupata chakula kila siku upo kutokana na misada ambayo tumepata” alisema Rehema.

Kwa upande wake Shaban Ally ambaye ametoa misaada hiyo kwa niaba ya Talib Hilal na Global Publishers amesema:- “ Kocha Talib Hilal na Global Publishers watoa msaada huu kwa kuzingatia kwamba hawa watoto wanaishi kwenye mazingira magumu hivyo nawaomba wasimamizi wa kituo hiki watumie hii misaada kama ilivyokusudiwa. 


“Tunampongeza sana Kocha Talib kwa moyo wake wa upendo kwa watoto hawa,” aliongeza

SOMA NA HII  SIMBA NAE AJIOKOTEA KIBONDE WAKE ...... SIO KWA KIPIGO HIKI