Home Uncategorized SENZO – TULIENI..MAMBO MAZURI YANAKUJA MSIMBAZI

SENZO – TULIENI..MAMBO MAZURI YANAKUJA MSIMBAZI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba wamekuwa wakihusishwa kuwafuatilia wachezaji mbalimbali ndani na nje ya nchi hasa Bara la Afrika.

Simba inapanga kufanya usajili wa maana ili kuwa na kikosi bora kwa ajili ya mashindano ya ndani na nje.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema hawana wasi wasi wowote kwani wana timu kubwa ya watu wenye uweledi katika masuala ya usajili na wameanza kufanya kazi hiyo muda mrefu wakishirikiana na benchi lao la ufundi chini ya kocha, Mbelgiji Sven Vandernbroeck.

Senzo amesema mara baada ya dirisha la usajili kufunguliwa wataweka wazi usajili wao kwani ni lazima wasajili kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na mapungufu.

Amesema wana majina ya wachezaji mkononi ambao wapo kwenye mpango wa kuwasajili kwani wanasubiri msimu umalizike na usajili ufunguliwe.

“Nadhani kama tutafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi na Kombe FA, kama malengo yetu yalivyo litakuwa jambo rahisi kwetu kupata wachezaji wazuri wenye uwezo wa kushindana katika ngazi ya Afrika kutokana na uwepo wa tiketi ya kucheza mashindano makubwa ngazi ya klabu ambayo kila mchezaji anayatamani kucheza,”
amesema.

SOMA NA HII  HII NDIYO HATMA YA NEYMAR NA PSG