Home Taifa Stars KOCHA TAIFA STARS APELEKEWA MAJINI…KUINGIA NAYO KAMBINI…VIMEMO VYATUMIKA KUITA STARS

KOCHA TAIFA STARS APELEKEWA MAJINI…KUINGIA NAYO KAMBINI…VIMEMO VYATUMIKA KUITA STARS

KOCHA TAIFA STARS APELEKEWA MAJINI...KUINGIA NAYO KAMBINI...VIMEMO VYATUMIKA KUITA STARS

Siku chache zilizopita Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, lilimtangaza Kocha Mpya wa Timu ya Taifa Mbeligiji mwenye asili ya Algeria Adel Amrouche.

Licha ya ugeni wake Machi 13 aliita kwa mara ya kwanza kikosi cha Timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu AFCON.

Sasa mchambuzi wa Soka nchini Oscar Oscar haamini kwamba Kocha huyo amepata wasa wa kuwatazama wachezaji na badala yake anapelekewa majini ili aite kwa ajili ya kuingia kambini pasipo yeye mwenyewe kujiridhisha.

Mzee wa Kaliua Oscar oscar anasema ifike wakati itengwe fedha kwa ajili ya Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ili kwenda kuwaangalia wachezaji wa Stars waanaocheza nje na wale wanaocheza mikoani ili Kocha asiwe anaita timu kwa kutumia vimemo.

SOMA NA HII  MECHI YA STARS V KENYA YAFUTWA, MECHI ZA NDANI KUSIMAMA NDANI YA WIKI MBILI