Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA FEI TOTO NA YANGA…FATUMA KARUME AIBUKA NA HILI JIPYA…ADAI...

KUHUSU ISHU YA FEI TOTO NA YANGA…FATUMA KARUME AIBUKA NA HILI JIPYA…ADAI TFF WANALAZIMISHA…

Habari za Yanga

Mwanasheria wa Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema ni mapema mno kuzungumza lolote kwa sasa, kufuatia maamuzi yaliyotangazwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Feisal aliomba kurejewa kwa maamuzi ya shauri lake dhidi ya Yanga, lakini bado Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaendelea kusimamia msimamo wake wa kumtambua kama Mchezaji halali wa Klabu hiyo ya Jangwani.

Fatma Karume ambaye alikuwa sehemu ya Wanasheria wa Kiungo huyo katika marejeo ya Shauri la Feisal dhidi ya Yanga, amesema wanachosubiri kwa sasa ni nakala ya hukumu ili taratibu nyingine zifuate ikiwa pamoja na kumshauri mteja wake.

Amesema jambo kubwa na la msingi katika kesi hiyo, ni mteja wake kulazimishwa kuendelea kuitumikia Yanga, ili hali yeye mwenyewe hataki kufanya hivyo, na TFF kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wanapaswa kuzingatia suala hilo.

“Tunasubiri nakala ya hukumu kutoka TFF na kisha nitamshauri Fei Toto kama maamuzi yake yatabaki hivyo tutaenda CAS.”

“Tatizo la TFF ni kumlazimisha Fei Toto kucheza Yanga kinyume na sheria za FIFA.. huwezi kumlazimisha mchezaji kucheza Yanga sio mtumwa yule.”

“Kama Yanga wanajua Fei Toto kavunja kinyume na utaratibu maana yake tayari mkataba haupo hivyo TFF wanatakiwa kutoa adhabu kama ni faini au kufungiwa miezi minne kwa mujibu wa sheria za FIFA na sio kumlazimisha mchezaji kucheza Yanga sio mtumwa.” amesema Fatma Karume.

SOMA NA HII  FT:- SIMBA 1-0 WYDAD....BALEKE AZIDI KUSHANGAZA SOKA LA TZ...WAARABU WAFURA KWA HASIRA...

1 COMMENT

  1. Nimekua napita maoni ya wengi kuhusu sakata la Feisal wakihoji maamuzi ya TFF na kuyaona sio sahihi ama yanamlazimisha Feitoto kuchezea Yanga wakati yeye hamtaki na wanasheria pia niliowaamini nao wameungana kuwaza kwamba, TFF wampige Tu faini Feitoto alipe aende zake,na mwana siasa mmoja pia ambaye Ni Mwanasheria pia. Nilichoona hapa,kumbe hatuna wanasheria Taaluma,Tuna wanasheria Vyeti.kumbe wao wangeamua hivyo.Lakini wajiulize ” Hivi ingekua Ni Club inamsajili mchezaji Leo miaka mfano 3 kisha miezi sita ijayo wakasema hutufai nenda unakotaka,na Hana soko, TFF tupige fain club tulipe huyu ainde zake hatumtaki,kama tunavyofukuza makocha. Wachezaji wangapi clubs zingeua vipaji vyao?. Nawashukuru TFF mnafanya maamuzi mkitafakari Kwa kina na kujali haya maana maamuzi ya hivyo Leo,kesho yataleta shida kubwa Sana.
    Feitoto ,Kubali kuelimishwa Mwanangu, wachana na washauri uchwara wanasimamia maslahi Yao.Yanga wanaumia lkn wewe unapoteza zaidi ya maumivu Yao.Mwambie Mama awe Mpole.Rudi Club,ongea na uongozi,anaekutaka aende Yanga,watakaa Mezani wataongea,Yanga watakuacha uende na Baraka zote.ndio utaratibu.acha kuongea mbovu itakugharimu.uko na thamani kwakuwa uko Yanga lkn ukiwa Nje watashuka Bei,Nunulika ukiwa ndani ya Yanga,utakuja kuniambia.