Home Habari za michezo MAKOSA YAWATESA RUVU SHOOTING…KOCHA MKUU AFUNGUKA…ISHU NZIMA IPO HIVI A-Z

MAKOSA YAWATESA RUVU SHOOTING…KOCHA MKUU AFUNGUKA…ISHU NZIMA IPO HIVI A-Z

MAKOSA YAWATESA RUVU SHOOTING...KOCHA MKUU AFUNGUKA...ISHU NZIMA IPO HIVI A-Z

Ruvu Shooting imekubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Mbeya Ciy katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa wenye lengo la kujiandaa na mechi tofauti kwa timu hizo.

Mbeya City inajiandaa na mechi yake ya robo fainali ya kombe la shirikisho, (ASFC) dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Aprili 2, huku Ruvu Shooting wao wakijiwinda dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Aprili 9.

Maafande hao ambao wapo nafasi mbili za mkiani kwenye ligi kwa pointi 20 wameweka kambi yao jijini hapa na leo chini ya bechi la ufundi likiongozwa na kocha mkuu, Mbwana Makata ilijikuta ikiloa kwa kisago hicho.

Katika mchezo wa ligi kuu, timu hizo zikicheza kwenye uwanja huo, City ilichakazwa mabao 2-1 na leo ni kama imelipa kisasi dhidi ya Maafande hao baada ya kuibuka na ushindi huo mnono.

Mabao ya City yamewekwa wavuni na Brown Mwankemwa dakika 16, Eliud Ambokile dakika ya 22, Richardson Ngy’ondya dakika ya 77 na Baraka Mwalubanju dakika ya 88 huku la kujifariji kwa Ruvu likifungwa na Mgandila Shaban dakika ya 30.

Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata amesema ishu haikuwa ni matokeo, bali kuangalia uimara wa kikosi chake kwa mchezaji mmoja mmoja na kwamba anaendelea kukisuka kabla ya mechi ijayo.

“Makosa bado yapo tumekosa hadi penalti lakini pia tumefungwa, naendelea kupambana kuhakikisha nasahihisha upungufu ili mchezo ujao tuweze kushinda na kujiweka pazuri,” amesema Makata.

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema matokeo hayo yanawapa mzuka katika kujiwinda na mechi ijayo ya robo fainali dhidi ya Singida BS na kwamba msimu huu baada ya kukosa nafasi nne za juu kwenye ligi kuu, wanaelekeza nguvu kwenye ASFC.

“Malengo yetu ni kucheza kimataifa na inawezekana, japokuwa kwenye ligi kuu tumeshakwama hivyo tunaenda kupambania kwenye kombe la shirikisho kimsingi ni kufikia ndoto zetu,” amesema Mwamlima.

SOMA NA HII  YANGA -TUNATAKA CHANGAMOTO YEYOTE..... ANAETUWEZA AJE...