Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana amesema Serikali itatoa Sh500 milioni kwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikiwa itafuzu kucheza fainali za mashindano ya Afcon 2023.
Dk Chana amesema Serikali imejipanga vyema kuwaunga mkono wachezaji wa timu ya Taifa ili kuhakikisha wanafanya vizuri.
Amesema kuwa wachezaji wamejipanga vilivyo hivyo serikali haina budi kutoa ushirikiano kwa hali na mali.
βNaibu Waziri Hamis Mwijuma atakwenda kutuwakilisha Wizara ya Michezo kwa ujumla na ataelekea Misri kuungana na wachezaji na mashabiki watakaoweza kuhudhuria katika mchezo huo dhidi ya Uganda,β
βNawaomba Mashabiki wafike kwa wingi hata siku ya mechi ya marudiano kwani wao ni wachezaji namba 12 na uwepo wao ni faraja kwa wachezaji wetu.β