Home Habari za michezo OKWA WA IHEFU APANIA KUWAUMBUA SIMBA KWA KUMUACHA DIRISHA DOGO…ISHU YAKE IKO...

OKWA WA IHEFU APANIA KUWAUMBUA SIMBA KWA KUMUACHA DIRISHA DOGO…ISHU YAKE IKO HIVI…

Okwa Akiwa Ihefu

Kiungo mshambuliaji wa Ihefu, Nelson Okwa amesema kikubwa kwake ni kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi zilizosalia ili kuhakikisha anaonyesha kiwango cha kusaidia timu yake.

Okwa anacheza kwa mkopo Ihefu, akitokea Simba iliyomsajili kutoka Rivers United, lakini hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Wanamsimbazi, hivyo akaona aende timu anayoweza kucheza.

Baada ya kutua Ihefu, Okwa amefunga bao moja dhidi ya Dodoma, hivyo anatamani kufunga zaidi kadri atakavyopata nafasi ndani ya kikosi hicho.

“Kikubwa kwangu ni nafasi ya kucheza, ili nifanye kitu kwenye mechi zilizosalia kumaliza msimu huu ambao sikuuanza vizuri,” alisema.

Alikiri Ihefu ina wachezaji wazuri na wazoefu ambao wanaibua ushindani unaompa chachu ya kuendelea kupambana zaidi kwa ajili ya kumalizia msimu akiwa kwenye kiwango kikubwa.

“Ni kiu ya kila mchezaji kufanya vizuri, kwa sababu soka ni kazi yake, hivyo unapokuwepo ushindani inakuwa sababu ya kuongeza umakini na kupambana kuhakikisha uwepo wangu unakuwa msaada kwenye timu,” alisema.

Kocha wa timu hiyo Zuber Katwila alisema “Wachezaji walioingia dirisha dogo wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho ,wanasaidiana na waliopo kuiondoa timu kwenye hatari ya kushuka daraja.”

SOMA NA HII  KISA MWAMUZI KUSHINDWA KUMPA INONGA KADI NYEKUNDU DHIDI YA YANGA...TFF WAIBUKA NA UTETEZI HUU MUJARABU....