Home Azam FC PRINCE DUBE NI HATARI…UJANJA WAKE NDANI YA 18

PRINCE DUBE NI HATARI…UJANJA WAKE NDANI YA 18

[the_ad id="25893"]

Ujanja wa Prince Dube muuaji anayetabasamu kutupia ndani ya ligi ni akiwa ndani ya 18 ambapo katupia kamba tano akiwa eneo hilo huku akitupia moja akiwa nje ya 18.

Dube nyota wa Azam FC mwenye mabao sita alifungua ukurasa wa kutupia mabao dhidi ya Kagera Sugar ilikuwa Uwanja wa Azam Complex, Agosti 17, 2022 dakika ya 17 Bao la pili alimtungua Aishi Manula Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Oktoba 27,2022 dakika ya 34 bao hili lilitibua mipango ya Simba kusepa na pointi na ukiwa ni mchezo pekee wa timu hiyo kupoteza msimu huu.

Ihefu walifuata kupewa tabu ilikuwa dakika ya 54 Uwanja wa Azam Complex, Oktoba 31,2022, Desemba 21,2022 aliwatungua Geita Gold Uwanja wa Nyankumbu dakika ya 14.

Mbeya City aliwatungua dakika ya 50 Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Desemba 31, 2022. Bao lake pekee ndani ya 2023 ni dhidi ya Simba alipomtungua kwa mara nyingine Manula sekunde ya 15 likiwa ni bao lake pekee alilofunga akiwa nje ya 18 akitumia mguu wa kulia.

Kwenye mabao hao ametupia matatu akiwa Uwanja wa Azam Complex na mawili akiwa Uwanja wa Mkapa na timu aliyoitungua mabao mengi ni Simba ambayo ni mawili.

SOMA NA HII  BAADA YA MAKI KUONDOKA ....SIMBA WAANIKA MUSTAKABALI WA 'STRAIKA MZUNGU'...WADAI HALIPO KWENYE MAKUBALIANO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here