Home Habari za michezo YANGA KUFANYIWA SAPRAIZI HII…HAIJAWAHI TOKEA BONGO…MABOSI WAPAGAWA

YANGA KUFANYIWA SAPRAIZI HII…HAIJAWAHI TOKEA BONGO…MABOSI WAPAGAWA

YANGA KUFANYIWA SAPRAIZI HII...HAIJAWAHI TOKEA BONGO...MABOSI WAPAGAWA

MWANZA. WAKATI Yanga ikikabiliwa na ratiba ngumu ya mechi za Ligi Kuu, Shirikisho (ASFC) na Kombe la Shirikisho Afrika, wapinzani wao Kagera Sugar watakabiliana nao mchezo ujao wa ligi wanajifua vikali ili kuwafanyia sapraizi ya maana.

Yanga itavaana na Kagera Sugar katika mchezo wa raundi ya 26 Ligi Kuu Aprili 11, saa moja jioni kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam ambapo katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa CCM Kirumba, Mwanza Yanga ilishinda 1-0 bao likifungwa na Walid (Clement) Mzize.

Kabla ya kukutana na Kagera Sugar, Yanga itakuwa bize na mchezo wa mwisho dhidi ya TP Mazembe Aprili 1 na kurejea nyumbani kukipiga na Geita Gold kwenye robo fainali ya ASFC, huku Kagera ikipumzika tangu ilipocheza Machi 9, dhidi ya KMC jijini Dar es Salaam.

Beki wa kati wa Kagera Sugar, Laurent Alfred ambaye alikosekana mchezo dhidi ya KMC waliochapwa mabao 2-0, alisema baada ya kurejea kambini Machi 21, benchi la ufundi limesisitiza zaidi kuhusu kujituma na kujitoa kwenye mazoezi ili kuhakikisha wanarekebisha makosa.

SOMA NA HII  KOSA LA MSIMU ULIOPITA....HIVI NDIVYO YANGA WANAVYOLIPIKA TENA MSIMU HUU BILA KUJIJUA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here