Home Habari za Simba SIMBA ACHENI KUMKANDAMIZA MZAMIRU…ALIPWA MSHAHARA MDOGO KULIKO SAWADOGO

SIMBA ACHENI KUMKANDAMIZA MZAMIRU…ALIPWA MSHAHARA MDOGO KULIKO SAWADOGO

Achana zile Assist za Clatous Chama acha na ile mikimbio na press za Ntibazonkiza acha na zile Hat trick za Beleke ila pale Simba SC Tanzania yupo mwana Kigoma anaitwa Mzamiru Yassini.

Huyu katika michezo mingi ya Simba ndio amekuwa kiini cha mipango yote ya mchezo uwanjani…ukimuona chama ana fent ukimuona Ntibazonkiza ana drible mpira basi ujue mpango wa kwanza unaanzia kwa Mzamiru.

Ubora wake kwenye kukaba njia kupokonya mipira na kusogeza pass kwa wakina chama ndio kiini cha ushindi katika kikosi cha Simba.

Mzamiru ile Energy yake pale Lunyasi labda inaweza kukaribiwa na Zimbwe jr ila sio ndani na nje ya Simba kama kuna kiungo wa kariba hii.

Dakika 180 timu ya taifa dakika 90 vs Raja pale Mohammed V kisha dakika 90 Azam complex ni ishara ya ubora na nishati ya kutosha.

Jana tumeona AISHI SALUM MANULA akiomba sub Inonga akitepeta Onyango akipoteza umakini ila Mzamir wa juzi, jana ndio yule wa leo na kesho.

Ila licha ya ubora wote ndani ya kikosi cha Simba sc Mzamir sio kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba sc pia sio rahisi kumuona Mzamiru akipostiwa kwenye kurasa za Simba sc ila usishangae kusikia Mzamiru analipwa pesa ndogo kuliko Sawadogo.

May be vijana wetu wa kitanzania wana shida kwenye negotiation wakati wa kusaini mikataba ila ifike muda vilabu vyetu navyo vione namna ya kutengeneza chapa za wachezaji wazawa.

Pale England sio tu kuwa wachezaji wa Kingereza wana mawakala bora ila tayari vilabu vya England vimeset standard za Fee na mishahara ya wachezaji wa Kingereza pia wameamua vilabu kutengeneza thamani ya wachezaji wa Kingereza.

Huyu Mzamiru kama ingekuwa sio mzawa angeimbwa na kupostiwa kila mahala ila kwa kuwa ni mzawa hata kwenye social media za Simba sc hana nafasi….. Tanzania ni muda sasa wa kuwapa thamani wachezaji wazawa.

SOMA NA HII  BAADA YA MAMBO KUWA SI MAMBO ....KANOUTE NAYE ASEPA SIMBA...ATAKA MAMILIONI KURUDI TZ....