Home Habari za michezo KOCHA RIVERS ATOA KAULI HII YA KEJELI DHIDI YA YANGA…”HAWANA UWEZO...

KOCHA RIVERS ATOA KAULI HII YA KEJELI DHIDI YA YANGA…”HAWANA UWEZO WOWOTE

KOCHA RIVERS ATOA KAULI HII YA KEJELI DHIDI YA YANGA...

Kocha Mkuu wa Rivers United, Stanley Eguma, ameibuka na kutoa kauli ya kejeli kwa wapinzani wake Yanga inayonolewa na
Nasreddine Nabi akisema anachokifikiria kwa sasa ni kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwa ndiyo kitu pekee cha msingi kwake.

Kauli ya Eguma imekuja ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwapanga Rivers kucheza dhidi ya Yanga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Mchezo wa kwanza
unatarajiwa kupigwa Aprili 23, mwaka huu nchini Nigeria, marudiano Aprili 30, mwaka huu jijini Dar.

Akizungumza nasi, Eguma alisema malengo yake makubwa ni kuona wanacheza fainali ya michuano hiyo msimu huu, hivyo hawezi kuona ugumu wa kucheza na timu yoyote katika hatua waliyofika kwa sasa.

“Sina sababu ya kufikiria juu ya mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Yanga kwa sababu ni timu ambayo tunaifahamu, tulikutana msimu uliopita na kuwatoa, kitu kikubwa ambacho nataka kuona nafika fainali msimu huu.

“Yanga siyo timu mbaya, Kama wapinzani lazima tuwape heshima, lakini sioni sababu yoyote ya wao kuharibu mipango yetu na tushindwe kufikia malengo,” alisema Eguma.

SOMA NA HII  JOHN BOCCO NDIO BASI TENA BENCHIKHA AMKATAA HADHARANI