Home Habari za michezo YALIYOMKUTA ACHRAF HAKIMI…YAMNYEMELEA C.RONALDO…ISHU NZIMA IKO HIVI

YALIYOMKUTA ACHRAF HAKIMI…YAMNYEMELEA C.RONALDO…ISHU NZIMA IKO HIVI

YALIYOMKUTA ACHRAF HAKIMI...YANAMNYEMELEA C.RONALDO...ISHU NZIMA IKO HIVI

Uhusiano wa mapenzi wa mwanasoka Cristiano Ronaldo na
mchumba wake Georgina Rodriguez unaripotiwa kuwa na doa, huku wakianza kukumbana na mawimbi.

Uvumi wa sasa ni kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Ureno, Noite das Estrelas, ambapo mwanasaikolojia, mwandishi wa habari na rafiki wa karibu wa familia hiyo walialikwa kutoa maoni yao kuhusu uhusiano wa Ronaldo.

Kama ilivyoripotiwa na Marca, mwanasaikolojia Quintino Aires alitoa maoni kwamba mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or hana raha katika uhusiano wake.

Kwamba maisha yake ya kibinafsi hayana furaha na kwamba kadiri anavyojitenga na mama yake,

Dolores Aveiro, ndivyo anavyopungua kuwa na hasira. Na sote tunajua kwa nini anazidi kuwa mbali na familia yake.” Alisema Aires.
Daniel Nascimento, ambaye nimwandishi wa habari, alikubaliana na matamshi ya Aires akisema:

“Ronaldo hana furaha. Georgina anatumia muda wake mwingi sokonihuko Riyadh na hiyo ndiyo sababu mojawapo inayomfanya Cristiano hana raha akiona hilo halifai. Anatumia pesa vibaya. Na
mbaya zaidi, anafikiria kuwa yuko sawa kiwango cha Cristiano. Anajiweka juu na hapendi kabisa.”

SOMA NA HII  SIMBA HAJAKATA TAMAA KWA MPANZU...DILI LAO LIMEFIKIA HUKU