Home Habari za michezo BARCELONA KUMREJESHA MESSI…WAANDAA DONGE HILI NONO…HACHOMOI!!!

BARCELONA KUMREJESHA MESSI…WAANDAA DONGE HILI NONO…HACHOMOI!!!

BARCELONA KUMREJESHA MESSI...WAANDAA DONGE HILI NONO...HACHOMOI!!!

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi anataka kurejea Barcelona lakini klabu hiyo ya Uhispania inahitaji kuongeza pauni milioni 88 kupitia mauzo ya wachezaji na kuamsha ‘kichocheo kingine cha kiuchumi’ ili kumsajili tena nahodha huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 (Mail)

Manchester United wanaimarisha juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane msimu huu wa joto, huku nahodha huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kutosaini mkataba mpya na klabu yake ya utotoni. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha amepewa mkataba mpya wenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki na The Eagles. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 unamalizika mwishoni mwa msimu huu, na kuzivutia Arsenal, Chelsea na Paris St-Germain. (Guardian)

AC Milan wameweka bei ya pauni milioni 35 kwa mlinda mlango wa Cameroon Andre Onana, huku Chelsea ikiripotiwa kumnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Goal)

Mshambulizi wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang, 33, ndiye anayelengwa zaidi na Barcelona kurejea Nou Camp msimu huu wa joto ili kumsaidia mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Liverpool Roberto Firmino, 31, ana nia ya kujiunga na Barcelona mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu – lakini klabu hiyo ya Uhispania haina nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Marca)

Kiungo wa kati wa Brighton Alexis Mac Allister, 24, ataondoka Seagulls msimu huu wa joto lakini anapanga kusalia kwenye Ligi ya Premia. Liverpool wanaongoza mbio za kuwania mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina, lakini Tottenham, Chelsea na Newcastle pia zimeonesha nia ya kutaka kumsajili. (90Min)

Kiungo wa kati wa Uhispania Gavi, 18, ameihakikishia klabu ya Barcelona kuwa hana mpango wa kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto, licha ya kuwa bado hajakubali mkataba mpya na anafuatiliwa na vilabu kadhaa barani Ulaya, ikiwemo Chelsea. (Sport)

Manchester City itamenyana na Manchester United, Liverpool na Tottenham kumsajili beki wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26, kutoka Napoli kwa £40m. (Sun)

Beki wa Uhispania Aymeric Laporte, 28, hana furaha Manchester City baada ya kutatizika kuanza mechi mara kwa mara na anataka kujiunga na Barcelona. (Relevo – kwa Kihispania)

Newcastle United wanapanga kumrejesha winga wa zamani wa Leeds United wa Barcelona Raphinha kwenye Ligi ya Premia. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuunganishwa St James’ Park na mlinzi wa Uturuki Arda Guler, 18, na kiungo mwenzake Ferdi Kadioglu, 23, kutoka Fenerbahce. (Mirror)

Newcastle United na Borussia Dortmund ni miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia hali ya winga wa Leeds Mholanzi Crysencio Summerville, 21. (Football Insider)

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Ureno Diego Moreira, 18, kutoka Benfica. (90Min)

Maskauti wa Newcastle na Manchester United walikuwa wakimtazama fowadi wa Slovenia Benjamin Sesko, 19, akiichezea Red Bull Salzburg wikendi. (Dakika 90)

Liverpool na Chelsea wameungana na Manchester City katika mbio za kumsajili beki wa kati wa Croatia Luka Vuskovic mwenye umri wa miaka 16 kutoka Hajduk Split. (Daily Mail)

Arsenal wanajipanga kufufua mpamngo wao wa kumnunua mshambuliaji wa Wolves kutoka Ureno Pedro Neto, 23. (TeamTalk)

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA UBINGWA YANGA....DICKSON JOB AZIDI KUFUNGUKA....AMTAJA MWAMNYETO...