Home Habari za michezo KOCHA YANGA AFICHUA KUMPIGA CHINI MORRISON…KUMBE ANA MAJERAHA HAYA

KOCHA YANGA AFICHUA KUMPIGA CHINI MORRISON…KUMBE ANA MAJERAHA HAYA

Habari za Yanga SC

Kocha msaidizi wa Yanga SC, Cedric Kaze amefichua kuwa sababu iliyowafanya benchi la ufundi kutomtumia winga Benard Morrison
kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya Rivers United.

Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini, mabao yaliowekwa kimiani na straika Fiston Mayele.

“Morrison alipata shida kidogo ya msuli kwenye mazoezi ya mwisho hapa Nigeria. Kama benchi la ufundi tukaona sio sawa kumlazimisha acheze kwani anaweza kuumia zaidi.

“Tuliamua kumuondoa kwenye mpango wa mechi ili kumpa nafasi ya kuwa sawa kabisa kwa ajili ya mechi zinazofata.

“Kila mtu anajua ubora wa Morrison akiwa na mpira na kwa mechi zilizobaki tunahitaji sana awe kwenye utimamu wake kwa asilimia 100 ili aweze kuwa na faida kwa timu,” alisema Kaze.

SOMA NA HII  DILI LA IDUMBA KUTUA SIMBA LIMEFIKIA HATUA HII...UNAAMBIWA NI BEKI HASWA...MAYELE HAPITI...