Home Habari za michezo SIMBA YAANDIKA REKODI HII MPYA…WAKONGWE WA SOKA WASHANGAZWA…ISHU NZIMA HII HAPA

SIMBA YAANDIKA REKODI HII MPYA…WAKONGWE WA SOKA WASHANGAZWA…ISHU NZIMA HII HAPA

Habari za Simba

Oktoba 27, 2023 itabaki kwenye kumbukumbu za mastaa Simba kwa kuwa ulikuwa ni mchezo wao kwa kwanza kutunguliwa ndani ya msimu wa 2022/23 kwenye ligi.

Baada ya hapo ni mechi 17 mfululizo mastaa hao walicheza huku wakiwa hawajaambulia kichapo tena ikiwa ni dakika 1,530.

Hapa SOKALA BONGO tunakuletea namna msako ulivyokuwa kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ndani ya ligi namna hii;
USHINDI

Simba imesepa na ushindi kwenye 13 ambazo ni dakika 1,170 na imepata sare mechi 4 ambazo ni dakika 360 mchezo wao ujao wa ligi utakuwa dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Highland Estate.

Ihefu sio watu wazuri waliwatibulia watani zao wa jadi Yanga mwendo wao wa kutofungwa kwenye mechi za ligi 49, dakika 90 Aprili 10 zitaamua kama nao watatunguliwa ama watakuwa wababe.

MABAO YA KUFUNGA 46
Ni mabao 46 wamefunga kwenye mechi 17 ambazo wamecheza wakiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 33.
Ukuta wao umetunguliwa mabao 10 ikumbukwe kwamba hii ni mara baada ya kutunguliwa na Azam FC. Jumla Simba imeruhusu mabao 14 baada ya kucheza mechi 24.

WALIWATUNGUA MENGI
Ubao wa Uwanja wa Mkapa Oktoba 30 ulisoma Simba 5-0 Mtibwa Sugar ikiwa ni mara aada ya kutoka kuonja joto ya jiwe kwa kuyeyusha pointi tatu mazima.

Timu nyingine ambayo ilikutana na kichapo hicho ilikuwa Geita Gold 0-5 Simba Desemba 30 2022 ile funga mwaka ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 7-1 Tanzania Prisons.

Mchezo huu unashikilia rekodi ya kukusanya mabao mengi ambayo ni 8 kwa msimu huu. Timu nyingine iliyotunguliwa ilikuwa Simba 4-0 Ruvu Shooting.

MWENDO WA TATU TATU
Sita zimepokea mabao matatumatatu zilipokutana na Simba na kuacha pointi tatu mazima uwanjani ilikuwa:- Polisi Tanzania 1-3 Simba, Coastal Union 0-3 Simba, KMC 1-3 Simba, Simba 3-2 Mbeya City, Simba 3-1 Singida Big Stars na Mtibwa Sugar 0-3 Simba.

KIKOMBE CHAAZAM FC
Tatu zilikutana na adhabu ya kikombe walichopewa na Azam FC kwa kutunguliwa bao moja kama walivyotunguliwa wao na kushindwa kurejesha ilikuwa; Simba 1-0 Ihefu, Simba 1-0 Namungo na Dodoma Jiji 0-1 Simba.

DAKIKA 360 WALITOSHANA NGUVU
Kwenye dakika 360 ngoma ilikuwa ngumu kwao na wapinzani kusepa na pointi tatu waligotea kugawana pointi ilikuwa; Singida Big Stars 1-1 Simba, Mbeya City 1-1 Simba, Kagera Sugar 1-1 Simba na Simba 1-1 Azam FC.

NAFASI Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 57 imecheza mechi 24 imetunguliwa mchezo mmoja pekee ambao ni dhidi ya Azam FC.

Ni mechi 17 wamesepa na ushindi jumlajumla huku wakiambulia sare sita kibindoni na safu yao ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 58 ikiwa ni namba moja kwa safu yenye mabao mengi.

SOMA NA HII  KUHUSU KIMATAIFA SIMBA ,YANGA NJIA HII HAPA