Home Habari za michezo KISA KAZI YA MAYELE …WAARABU WAINGIA MCHECHETO DAR…KOCHA WAO APATWA NA KIGUGUMIZI…

KISA KAZI YA MAYELE …WAARABU WAINGIA MCHECHETO DAR…KOCHA WAO APATWA NA KIGUGUMIZI…

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa US Alger ya Algeria ambao ni wapinzani wa Young Africans Abdelhak Benchikha amepatwa na kigugumizi kuwazungumzia wapinzani wake hao ambao watakutana kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika huku akisema kwa kifupi kuwa anatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa timu hiyo.

USM Alger walifanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwaondosha Asec Mimosas ya Ivory Coast na wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Yanga ambapo wataanzia ugenini kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar Mei 28 na kisha watamalizia kwenye uwanja wao wa nyumbani Juni 3 nchini Algeria.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, kocha Benchikha amesema kuwa anatarajiwa kupata upinzani mkubwa kutokana na kuwa ni mchezo wa fainali na huku akiweka wazi kuwa hakuna timu ambayo imetinga fainali itatamani kupoteza katika mchezo wa Fainali.

“Hakuna timu ambayo imetinga katika hatua ya fainali itatamani kuona kuwa inapoteza mchezo huo, hapo ndio ugumu wa mchezo huanza kuonekana kwa kuwa upinzani huwa ni mkubwa.”

“Hakuna fainali ambayo huwa nyepesi hivyo naamini tunakwenda kukutana na upinzani mkali kutoka kwa wenzetu, tunafahamu kuwa tunatakiwa kushinda lakini haitakuwa rahisi kama watu wanavyoona,” amesema kocha huyo

Miongoni mwa nyota wa Young Africans ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu katika kombe hilo ni Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele ambaye amefunga mabao sita akiwa na uhakika wa kubeba kiatu cha ufungaji bora wa michuano hiyo

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUONGOZA LIGI...GSM AGUNA KISHA AFANYA KUFRU BAB KUBWA HUKO...MWAKALEBELA ATIA NDIMU...