Home Azam FC BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAMTAKA AKAMINKO….MABOSI AZAM WAVUNJA UKIMYA…WAANIKA DILI LILIVYO…

BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAMTAKA AKAMINKO….MABOSI AZAM WAVUNJA UKIMYA…WAANIKA DILI LILIVYO…

Habari za Michezo

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Azam FC Abdulkarim Amin ‘Popat, amesema kiungo wa timu hiyo, Mghana James Akaminko bado yupo sana Azam na haondoki.

Popat amesema licha ya mchezaji huyo kuhitajika na baadhi ya timu, bado yupo kwenye mipango ya muda mrefu, ivyo hawapo tayari kumuweka sokoni kwa sasa.

“Ndio kwanza tumemsajili msimu huu, na sisi tuna shida naye, hatuwezi kumuachia kirahisi, halafu mwisho wa siku watu waendelee kuuliza Azam FC inakwama wapi?

“Hatuwezi kusema tunaijenga timu halafu tumuachie mchezaji bora, hiyo inakurudisha nyuma na kuanza moja, hata kama ni biashara ni lazima uangalie na mahitaji yako.”

Nyota huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa katikati ya dimba amekuwa akihusishwa na kutakiwa na timu mbalimbali nchini, huku baadhi zikitajwa kupeleka ofa rasmi ya kumtaka.

SOMA NA HII  MAMELODI SUNDOWN YAANDIKA HISTORIA BAADA YA KUTWAA UBINGWA AFL KWA KUICHAPA WYDAD