Home Habari za michezo DAKIKA 20 ZA GIZA MECHI YA YANGA VS RIVERS UNITED…TANESCO WARUKA WAFUNGUKA...

DAKIKA 20 ZA GIZA MECHI YA YANGA VS RIVERS UNITED…TANESCO WARUKA WAFUNGUKA HAYA

DAKIKA 20 ZA GIZA MECHI YA YANGA VS RIVERS UNITED...TANESCO WARUKA WAFUNGUKA HAYA

Shirika la Umeme (TANESCO) limesema baada ya Majenereta ya Uwanja wa Taifa kushindwa kufanya kazi katikati ya mechi ya Yanga vs Rivers United ya Nigeria na taa kuzimika, umeme wa TANESCO ndio ulianza kutumika na mchezo ukaendelea.

Umeme huo ulikatika kwa takribani dakika 20 wakati mchezo ukiwa dakika ya 24 na kufanya refa kusimamisha mchezo huku wachezaji wakilazimika kusubiri hali irejee kawaida ili mchezo uendelee.

“Tunasikitika kwa kadhia iliyojitokeza na tutashirikiana na wenzetu kwa siku za usoni jambo hili lisijirudie, Uwanja wa Taifa unahudumiwa na vyanzo viwili vya umeme ambavyo ni TANESCO na Majenereta ya uwanja, mechi ya leo uwanja ulikuwa unahudumiwa na majenereta ya uwanja” TANESCO.

Ikumbukwe pia kuwa, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon kati ya Taifa Stars na Uganda, taa hizo zilizima kwa zaidi ya dakika 30 kisha baadae tatizo hilo likarekebishwa na mechi
ikaendelea mpaka mwisho.

SOMA NA HII  ROBERTINHO:- WYDAD HAWATAAMINI MACHO YAO...MZAMIRU ATULIZA PRESHA...