Home Habari za michezo KIPA RIVER UNITED ANUKIA SOKA LA BONGO….ATAJA TIMU ANAYOTAKA KUICHEZEA…

KIPA RIVER UNITED ANUKIA SOKA LA BONGO….ATAJA TIMU ANAYOTAKA KUICHEZEA…

Tetesi za Usajili Bongo

Kipa wa Rivers United ya nchini Nigeria, Victor Sochima ameweka wazi malengo yake msimu ujao ni kucheza timu kubwa hapa Tanzania huku akitaja miongoni mwao zinazomvutia ni matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC.

Sochima alionyesha kiwango kizuri katika michezo yote miwili ya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga hali iliyozifanya baadhi ya timu nchini kuanza mazungumzo naye ya kimya kimya.

Akizungumza nasi kutoka Nigeria, Sochima alisema timu nyingi zimefurahishwa na uwezo wake hivyo zilimfuata kuzungumza naye ingawa kwa sasa akili yake ameiwekeza kwa ajili ya kuhakikisha msimu huu unaisha.

“Siwezi kuweka wazi kwenye kila kitu kinachoendelea lakini itoshe kusema ni kweli nimefuatwa na baadhi ya timu ikiwemo Yanga kwa sababu baada ya mechi yetu kuisha nilifuatwa na kocha wao, Nasreddine Nabi,” alisema.

Sochima aliongeza mbali na Yanga ila timu nyingine ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji saini yake ni Azam ambayo kwake binafsi anatamani kuichezea kwani miundombinu iliyonayo inamshawishi tofauti na kwingine. “Pale Azam kuna rafiki yangu mkubwa anaitwa, Isah (Ndala) ni mchezaji mzuri ambaye nimekuwa naye kwa ukaribu hivyo nitafurahia kama itatokea siku moja tutacheza wote pamoja ingawa kwa sasa dili bado halijakamilika.”

Wakati Sochima akiweka wazi mipango hiyo ila Mwanaspoti linatambua Azam iko kwenye rada za kutafuta kipa mwingine atakayesaidiana na Abdulai Iddrisu iliyemsajili Januari mwaka huu akitokea Bechem United ya kwao Ghana.

Usajili wa kipa mwingine ni kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha Ali Ahamada ambaye licha ya kuchukua kiasi kikubwa cha fedha tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu ila amekuwa akifanya makosa mengi ya kizembe.

Ahamada raia wa Comoro alijiunga na Azam Julai mwaka jana akiwa ni miongoni mwa makipa wazoefu kwani amewahi kuzichezea timu mbalimbali Barani Ulaya ikiwemo miamba ya Ufaransa, Toulouse ambayo inayoshiriki Ligue 1.

SOMA NA HII  MTUNISIA MWINGINE ASHUSHWA YANGA KUMWAGA WINO