Home Habari za michezo SAKHO AZIDI KUWAUMBUA WATU SIMBA ….AENDELEA KUTIKISA KWA REKODI HIZI…

SAKHO AZIDI KUWAUMBUA WATU SIMBA ….AENDELEA KUTIKISA KWA REKODI HIZI…

Habari za Simba

Msenegal Pape Sakho anayekipiga ndani ya kikosi cha Simba amevunja rekodi yake aliyoiandika yeye mwenyewe msimu wa 2021/22 kwenye suala la kutupia mabao.

Nyota huyo msimu huo alitupia mabao sita kimiani baada ya kucheza jumla ya mechi 22 akitumia dakika 1,355, alitengeneza pasi tano za mabao.

Mabao hayo sita ni matano alitumia mguu wa kulia huku bao moja alitumia mguu wa kushoto na yote alifunga akiwa ndani ya 18.

Msimu wa 2022/23 ni mabao tisa katupia akiwa amecheza mechi 23 akisepa na dakika 1,604 akitumia mguu wa kulia kufunga mabao yote na pasi ya bao katoa moja.

Sakho katupia mabao manne akiwa nje ya 18 na mabao matano akiwa ndani ya 18 hivyo kahusika kwenye jumla ya mabao 10 yaliyofungwa na timu hiyo kati ya 66 yaliyofungwa na Simba.

Licha ya kutupia mabao hayo mengi Simba imegotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 mabingwa ni Yanga wenye pointi 74.

SOMA NA HII  KUHUSU KURUHUSU MAGOLI KIZEMBE...CHE MALONE AANIKA 'ISHU' YAKE NA INONGA....