Home Habari za michezo MABOSI SIMBA WAANZA KUYAPANGIA BAJETI MABILIONI YA CAF SUPER LEAGUE…BAJANA ATAJWA…

MABOSI SIMBA WAANZA KUYAPANGIA BAJETI MABILIONI YA CAF SUPER LEAGUE…BAJANA ATAJWA…

Tetesi za Usajili Simba

Viongozi wa Simba umesema mkwanja wanaotarajia kupata watafanya usajili mkubwa huku baadhi ya nyota wakitajwa akiwemo kiungo wa Azam FC, Sospeter Bajana kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kwa msimu ujao.

Bajana amehusishwa kujiunga na Simba baada ya mkataba wake na Azam FC kufikia ukingoni huku ikidaiwa kuwa hajaongeza mkataba na waajiri wake hao wapya ambao wako katika mazungumzo.

Ahmed Ally alisema kwa fedha wanazozipata kutoka CAF ikiwemo Super League na vyanzo vyao vingine vya fedha ikiwemo kwa mwekezaji wao Mohammed Dewji (Mo Dewji).

Alisema kulingana na fedha watakazozipata wanauwezo kwa kununua mchezaji yoyote hata kununua timu 15 zinazoshiriki Ligi Kuu nchini.

“Tumekuwa na mzigo mkubwa ikiunganisha fedha za mwekezaji wetu, Mohammed Dewji, vyanzo vya Simba pamoja na fedha za Super League hali hiyo tutafanya usajili mkubwa,” alisema Ahmed.

Kuhusu kiungo huyo wa Azam FC, Bajana, Ahmed alisema wako kwenye mawindo makali na wanaangalia watu kadha wa kadhaa kwa sasa wanaangalia kila sehemu ndani na nje ya nchini ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili kuifanya Simba kuwa bora zaidi.

“Tuko katika mawindo makali tunaangalia watu kadha wa kadha ndani na nje ya Tanzania, Bajana tunamkubalia sana ni kijana ambaye ni mzuri, kocha Robertinho (Roberto Oliveira) akipendekeza basi tutafanya mazungumzo na Azam kupata huduma yake,” alisema Ahmed

Alisema wanahitaji kuboresha kikosi chao kiwe imara na kutotaka kurudia waliyoyafanya kwa msimu uliopita na sasa kujiwema imara zaidia.

Aliongeza kuwa Joash Onyango bado yupo sana ndani ya klabu hiyo kwa kuwa ana mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano.

Ahmed alisema hawajapokea barua kutoka kwa mchezaji huyo akihitaji kuondoka ndani ya kikodi cha timu hiyo, kuna maneno yameenea kuwa Onyango ameandika barua hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa msimu huu lakini akaongeza mkataba na umebaki wa mwaka mmoja.

“Onyango bado yupo Simba kwa sababu ana mkataba wa mwaka mmoja na anaendelea kuitumikia klabu yake na msimu ujao atakuwa miongoni mwa sehemu ya kikosi chetu,” alisema Ahmed.

Katika hatua nyingine Uongozi wa Simb upo katika hatua za mwisho za kumpata skauti wao ambaye atakuwa na kazi ya kuleta wachezaji bora ndani ya klabu hiyo .

Uongozi umethibitisha kuwa skauti huyo anatoka kati ya nchi za Hispania ama uholanzi na atakuwa akishirikiana vyema na benchi la ufundi katika usajili.

Naye kiungo huyo wa Azam FC, Bajana amekiri kufuata na viongozi wa Simba na wako katika mazungumzo nao lakini pia anaendelea kuongea na wajiri wake wa sasa kuhusu kuongeza mkataba mwingine.

Alisema hadi sasa anafanya mazungumzo na viongozi wa klabu zote mbili na anachoangalia zaidi kwenye maslahi ambayo ataridhishwa nayo basi atachagua sehemu moja kubaki Azam FC au Simba.

“Sasa ni mapema kusema msimu ujao nitacheza wapi, kwa sababu mkataba wangu kwa sasa upo ukiongoni, nafanya mazungumzo na Azam FC kwa mkataba mpya lakini Simba wameonyesha nia.

Soka ni kazi yangu naangalia maslahi zaidi kwa sababu nina familia ambayo inanitegemea, je ni kubaki Azam FC au kwenda Simba ni suala la nani mwenye ofa nzuri,” alisema Bajana.

SOMA NA HII  TECNO YAGUSA HISIA: MCHEZO WA HISANI WACHOCHEA HAMASA YA KUBORESHA VIWANJA VYA JAMII BARANI AFRIKA