Home Habari za michezo YANGA WATAKA BILIONI 5 KUMUUZA MAYELE…MAMELOD, AL HILAL NA MAZEMBE KUTUMA OFA...

YANGA WATAKA BILIONI 5 KUMUUZA MAYELE…MAMELOD, AL HILAL NA MAZEMBE KUTUMA OFA NONO ZAIDI..

Habari za Yanga SC

Wakati tetesi zikisambaa kila kona kuhitajika nwa Vilabu vingi Barani Afrika kwa Mshambualiaji wa Yanga Fiston Mayele.

Afisa wa habari wa Yanga Ali Kamwe amevikaribisha vilabu vyote ambavyo vinamtaka mshambuliaji wao Fiston kalala Mayele waje wakae mezani wamalizane.

“Sisi Kama Yanga hatuwezi kumzuia Fiston kalala Mayele kwenda sehemu nyingine Ila thamani ya Fiston kalala Mayele kwa sasa ni Billion 5 kuvunja mkataba wake watu wasiogope hata mwakarobo Kama wanamuhitaji waje tumalizane tunachotaka tu utaratibu ufatwe”.

Tayari klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya kusini imeweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili Mayele kwa ajili ya kuimarisha safi yao ya ushambuliaji kwa  msimu ujao.

Hata hivyo, taarifa kutoka Sudani pia zinadai kuwa klabu ya Al Hilal inayonolewa na Mkongomani Frorent Ibenge nayo imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo.

Inaelezwa kuwa, maafisa wa Al Hilal walianza kumtupia macho Mayele baada ya mechi yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, ambapo Yanga walifungwa.

Lakini kama hiyo haitoshi , klabu ya TP Mazembe nao wanaelezwa kuwa wako mbioni kujaribu kumpata mshambulaiji huyo ambye mkataba wake na Yanga unakaribia ukingoni.

Mazembe ambao kuelekea msimu ujao wanajipanga kufanya usajili mkubwa wa kuwarudishia makali yao wamekusudia kutuma ofa nono ya kumshawishi Mayele kurudi nyumbani kucheza ligi ya Congo.

Tangu kujiunga kwake na Yanga, Mayele amekuwa na mchango mkubwa mno katika kuifanya timu hiyo kupata mafanikio waliyokuwa nayo hivi sasa.

Katika Msimu wake wa kwanza tu , alifanikiwa kuipa nafasi ya pili timu yake, huku yeye akiwa sehemu ya washambuliaji wlaiongoza kwa kufunga magoli kwa upande wa Yanga.

Kama hiyo haitoshi, Mayele pia amekuwa msaada mkubwa sana kwa Yanga kufika Fainal ya kombe la Shirikisho Afrika, kwani magoli yake yameifanya timu hiyo kuwa na safu kali ya kupachika mabao.

Hata hivyo, mara kadhaa Mayele ameshindwa kuweka wazi mustakabali wake ndani ya kikosi cha Nabi, ambapo amekuwa akisema kuwa anapambana kuona anaisidia timu kufika malengo kwanza.

SOMA NA HII  SIMBA YAANGUKIA KWENYE MTEGO HUU WA FIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here