Home Habari za michezo HII HAPA MASHINE YA KAZI KUTOKA ASEC MIMOSAS INAYOKUJA YANGA…SHABANI DJUMA ATAFUTE...

HII HAPA MASHINE YA KAZI KUTOKA ASEC MIMOSAS INAYOKUJA YANGA…SHABANI DJUMA ATAFUTE PAKWENDA..

Tetesi za usajili Yanga

Tetesi zinaeleza kuwa Yanga wanamfuatilia beki wa kulia wa ASEC MIMOSAS ya Ivory Coast, Yao Kouassi Attohoula mwenye umri miaka 26.

Beki huyo anasifika kwa uwezo mkubwa wa kukaba na kupandisha mashambulizi bila kusahau kupiga krosi za maana.

Msimu huu kwenye ligi ya Ivory Coast amefunga mabao 2 na pasi 7 za mabao huku kwenye Shirikisho akipiga pasi 3 za mabao.

Djuma Shabani inaelezwa kocha Nabi ameanza kuingiwa na mashaka juu ya uwezo wake katika siku za hivi karibuni kushindwa kuendana na kasi ya wapinzani jambo ambalo limepekea beki wa kati Dickson Job kupewa upande wa kulia.

Toka kuanza kwa msimu huu, Djuma akuwa kwenye kiwango kizuri hali iliyopelekea aliyekuwa kocha wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera kudai kuwa beki huyo amenenepeana mno.

Djuma alisajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitoka nchini Congo kwenye klabu ya AS Vita ambapo alikuja pamoja na Mayele, Bangala na Moloko.

Msimu wake wa kwanza Yanga ulikuwa wenye mafanikio ambapo alifanikiwa kucheza karibu mechi zote za kimashindano kabla ya kuanza kupata ushindani wa namba msimu huu.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUCHAPWA MOROCCO JUZI..MANARA ASHINDWA KUJIZUIA...ADAI 'WAMEPAKATWA KIBWEGE'..