Home Habari za michezo HUYU NDIYE NABI BANA….KAANZA USAJILI MAPEMAA….VYUMA HIVI VITATU VYA CAF KUTUA CHAP…

HUYU NDIYE NABI BANA….KAANZA USAJILI MAPEMAA….VYUMA HIVI VITATU VYA CAF KUTUA CHAP…

Habari za Yanga SC

Wakati Yanga wakiwa wamefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kuna jambo kubwa kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi pamoja na benchi la ufundi wanalifanya kwa ajili ya msimu ujao wa kimataifa.

Yanga jana walifanikiwa kutinga fainal ya kombe la shirikisho baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo Gallansts na kutinga fainali ya Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Katika kuhakikisha kuwa msimu ujao wanaendeleza walipoishia katika michuano ya kimataifa, kocha Nabi ameonekana kuanza safari ya  mapema kusaka majembe mapya kupitia michuano hiyo hiyo ambayo amekuwa akitumia staili ya aina yake.

Imeshuhudiwa kocha Nabi mara kwa mara baada ya michezo kumalizika akifanya mazungumzo na wachezaji ambao wamekuwa wakimvutia akiwa sambamba na meneja wa timu Walter Harryson jambo ambalo ni ishara nzuri kuelekea katika dirisha kubwa la usajili msimu ujao.

Mpaka sasa kwenye michuano ya kimataifa  kocha Nabi ameshafanya mazungumzo na wachezaji watatu ambao wote walionekana kuisumbua Yanga na wamefanya vyema katika michuano hiyo kama ifuatavyo.

KATLEGO OTLADISA- MARUMO

Mchezaji wa mwisho kwa kocha Nabi kuonekana akizungumza naye ni Katlego Otladisa kutoka Marumo Gallants katika mchezo ambao Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Katika mchezo huo, Otladisa alikuwa amevaa jezi namba 11, aliwasumbua sana Yanga kutokana na spidi yake na chenga jambo ambalo baada ya mechi kumalizika Nabi alimtuma Meneja Walter Harryson kuzungumza naye na alionekana akimuomba namba yake.

MORRICE CHUKWU – RIVERS UNITED

Chukwu ni kiungo mkabaji lakini akiwa anaweza pia kucheza kama kiungo mshambuliaji. Mchezaji huyu baada ya kuonekana kuwavuruga viungo wa Yanga kama kawaida yao Nabi na meneja Walter walizungumza naye kwa dakika mbili jijini Dar.

Hali ambayo ilikuwa sio ya kawaida jambo ambalo liliashiria kuwa walikubali kazi yake huku pia meneja huyo alionekana kuwa na Simu akichukuwa mawasiliano yake.

CHEICKNA DIAKITE – REAL BAMAKO

Huyu ni winga wa Real Bamako ambaye katika mchezo ambao Yanga walikuwa ugenini nchini Mali alikiwasha sana kiasi cha Kocha Nabi kuzungumza naye baada ya mpira kumalizika.

Lakini hata baada ya mchezo wa marudiano wakiwa Dar bado kocha Nabi alikwenda tena kuzungumza na mchezaji huyo jambo ambalo lilionyesha kuwa huenda kuna mambo ya usajili yalikuwa yakiendelea kati yao.

SOMA NA HII  HUYU HAPA STAA WA YANGA ANAYETAKIWA NA MARSEILLE YA UFARANSA...MWINYI ZAHERA TOA LA MOYONI KUHUSU DILI HILO..