Home Azam FC WAKATI YANGA WAKIZUBAA NA KINA MAYELE….SIMBA NA AZAM MDOGO MDOGO WAANZA MAMBO…

WAKATI YANGA WAKIZUBAA NA KINA MAYELE….SIMBA NA AZAM MDOGO MDOGO WAANZA MAMBO…

Habari za Michezo leo

Klabu za Simba na Azam tayari zimeanza rasmi maandalizi ya msimu mpya baada ya kujua ni wapi wataenda kuweka kambi kwa ajili ya kujifua na kujiandaa na msimu ujao.

Azam ambayo inatarajia kurudi kambini Julai 3 katika viunga vya Chamazi na Julai 4 wataanza mazoezi kisha ndio wataondoka nchini kutimkia Tunisia.

Upande wa Simba yenyewe inatarajia kurejea kambini Julai 12 hadi 13 kisha itakuwa na siku kadhaa ya kuweka mambo sawa halafu watakwenda Uturuki kuanzia Julai 15.

Afisa Habari wa klabu ya Azam, Hasheem Ibwe ambaye almekiri timu yao itaenda kuweka kambi nchini Tunisia.

Ibwe alisema watakuwa na siku chache za kukaa nchini kisha wataondoka kwa ajili ya kwenda kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao.

“Tutaanza kuingia kambini Julai 3 na Julai 4 tutaanza mazoezi, tutaondoka tarehe 9 tutaondoka kisha tunatarajia kurudi tarehe 30 mwezi huo huo;

“Tutaondoka na wachezaji wote ambao wameshatambulishwa na wale ambao bado hawajasajiliwa nikimaanisha wapya watakuja moja kwa moja tutakapokuwa;

“Pia kutakuwa na baadhi ya wachezaji wazawa ambao watatambulishwa hapa hapa na wengine tukiwa tupo Tunisia.”

Upande wa Simba licha ya kwamba wamekuwa wagumu kutoa taarifa zao, chanzo kimoja kutoka ndani ya timu hiyo kililidokeza gazeti hili kwamba wataenda kuweka kambi nchini Uturuki.

“Sisi hatutokuwa na muda mrefu kule Uturuki kwa sababu tuna Ligi hapa ya Super Cup kwahiyo tutaenda kujiandaa na Ligi hiyo na mashindano mengine, baada ya hapo tutaendelea na ratiba zetu zingine,”kilisema chanzo hicho.

Azam msimu uliopita iliweka kambi nchini Misri huku Simba ikiwa Morocco.

Wakati huo huo klabu ya Singida Fountain Gate ambayo ilikuwa inaitwa Singida Big Stars inatarajiwa nayo kwenda kuweka kambi nchini Tunisia baada ya kusaini mkataba wa kualikwa na timu ya US Monastir.

SOMA NA HII  BAADA YA KUKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI....NABI APIGA 'STOP' ...AMKINGIA KIFUA MCHEZAJI WAKE...