Habari za Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU CHAMA NA KUONGEZA MKATABA SIMBA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…

admin June 24, 2023 12:06 pm

Meneja wa Habari na Mawasilino wa SImba SC Ahmed Ally amefichua kufikiwa kwa makubalino kati ya Uongozi wa Klabu hiyo na Kiungo kutoka Zambia Clatous Chota Chama.

Pande hizo mbili zilikuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, kufuatia mkataba wa awali wa kiungo huyo kutarajia kufikia kikomo mwezi Januari 2024.

Ahmed Ally amefichua siri hiyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akieleza kuwa, Chama amekubali kusalia Simba SC, na atakaporejea nchini Tanzania atasaini mkataba mpya wa miaka miwili.

Chama alisaini mkataba na Simba SC mwezi Januari 2021 aliposajiliwa tena klabuni hapo akitokea RS Berkane ya Morocco, ambako alishindwa kucheza soka lake, kutokana na mazingira ambayo alidai hayakuwa rafiki kwake na familia yake.

Ahmed Ally ameandika: Chama amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuitumika Simba Sports Club

Mkataba utasainiwa akirejea Tanzania baada ya majukumu ya timu ya taifa na mapumziko kabla ya Pre Season.

MASHINE MPYA MSIMBAZI HIZI HAPA….MBRAZILI KAANIKA USAJILI WOTE ULIVYO… KUTOKA MKUTANO MKUU: YANGA WAVUNA BILIONI 7 ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “KUHUSU CHAMA NA KUONGEZA MKATABA SIMBA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…”

  1. Juma misalaba says:

    Msitu anime wanachama Simba sport club Kwa kubania fedha za usajili, mpaka tunazidiwa na hao,,,,,,,,,,,,,,,,,, watumwa wa fikra

Leave a Reply