Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- MAYELE ANAONDOKA YANGA HUO NDIO UKWELI…OFA IPO…

ALLY KAMWE:- MAYELE ANAONDOKA YANGA HUO NDIO UKWELI…OFA IPO…

Habari za Yanga

Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Ally Shaban Kamwe amesema kuna uwezekano mkubwa Mshambuliaji wao kutoka DR Congo Fiston Mayele akaondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha Dirisha la Usajili.

Mayele amekuwa akitajwa kuwindwa na baadhi ya Klabu za Barani Afrika na kwingineko, kufuatia uwezo mkubwa aliouonesha wakati wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2022/23, huku akiibuka kinara wa ufungaji Bora katika Michuano hiyo kwa kufunga mabao 7 akimuacha ranga Chivaviro wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini aliyefunga mabao 6.

Ally Kamwe amesema Young Africans imepokea ofa kadhaa hadi sasa zinazomuhusu Mshambuliaji huyo, lakini kabla ya kufanya maamuzi yoyote, Uongozi utakaa naye chini na kumpa ofa mpya, na kama mambo yatakuwa tofauti watakuwa tayari kumuachia aondoke ili akatafute maisha kwingine.

“Fiston Mayele kwa sasa yupo kwenye majukumu yake ya timu ya Taifa ya DR. Congo ila akirejea sisi tutampa ofa yetu ya kutaka kumuongezea mkataba kwenye ule mwaka mmoja uliobaki, ila kama hataridhishwa na ofa yetu tutamsikiliza nini anakipendekeza na kama atakuwa na ofa kubwa zaidi yetu tutaikaribisha mezani timu inayomuhitaji”

“Tumepokea ofa nyingi kutoka kwenye timu kubwa sana barani Afrika zinazomuhitaji Fiston Mayele ila sisi kama Klabu kipaumbele chetu ni Fiston Mayele abaki Tanzania kuendelea kula mema ya nchi yetu, ila kama mwenyewe hatotaka tutafuata taratibu zote za soka inavyotakiwa tutamruhusu aende alipopata ofa kubwa zaidi ya Yanga SC” amesema Ally Kamwe

Mbali na kutamba katika Michuano ya Kimataifa, Mayele pia ameonesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu msimu wa 2022/23, akimaliza Kinara wa ufungaji Bora sawa na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na klabu ya Simba SC Saido Ntibazonkiza, wakifunga mabao 17 kila mmoja.

SOMA NA HII  MALONE AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU YEYE KUTUA SIMBA